'Siwezi kuamini'Jamaa aliyedai kumchumbia Ngina Kenyatta azungumza baada ya Ngina kujifungua

Muhtasari
  • Jamaa aliyedai kumchumbia Ngina Kenyatta azungumza baada ya Ngina kujifungua
ngina-kenyatta2
ngina-kenyatta2

Hata baada ya kumwamndikia barua ya mapenzi Ngina Kenyatta, Shem kutoka Vihiga bado hajakata tamaa ya kumpenda  Ngina.

Shem alivuma mwezi wa juni baada ya barua yake kuenea sana mitandaoni, na kukiri upendo wake wa ngina.

Habari za binti wa Rais Uhuru Kenyatta, Ngina Kenyatta kujifungulia katika hospitali ya jiji zimewashangaza Wakenya wengi.

Mtu mashuhuri ambaye ameshtushwa sana na habari hiyo ni mmoja Beverton Mukalo; mtoto wa mkata miwa kutoka Kaunti ya Vihiga.

Miezi iliyopita, Shem aliandika barua ya upendo kwa binti ya rais, akimtaka amuoe.

Akiwa kwenye mazungumzo ya kipekee na Mpasho alisema kwamba hawezi amini habari za kujifungua za Ngina kama vile hakuamini za uchumba wake.

"Moyo wangu uliruka kwa mpigo nilishtuka siwezi kuamini! Wakati kulikuwa na uvumi kwamba alikuwa amepata mchumba sikuamini," alisema.

Bila kujali maendeleo ya sasa, Shem bado anatarajia kushinda moyo wa binti wa rais.

"Ninaamini bado niko kwenye kinyang'anyiro. Bilionea wa Uingereza Richard Branson alioa mkewe wa sasa wakati alikuwa ameposwa na mtu mwingine. Nitaendelea urusha mistari yangu," Shem alisema.

Alipoulizwa na mwandishi wa Mpasho Fridah kwanini anaamini kwamba yeye ni bora kuliko mwanamume mwingine yeyote alikuwa na haya ya kusema.

"Ninaleta mengi zaidi mezani, ujasusi, tamaa, mtu aliyejitengeneza, ni bilionea mtarajiwa. Upendo wangu kwake bado uko nguvu."

Mwezi wa Juni alisema barua yake ya mapenzi kwa Ngina ilikuja baada ya kuachana na mpenzi wake, na kwake, binti ya Rais ndiye mwanamke bora.

Anapenda utu na umaridadi ulioonyeshwa na Ngina Kenyatta katika hafla ambazo ameonekana katika umma.

"Nina shisia za kimapenzi kwake. Najua vizuri kwamba hiyo ni kulenga ngumi kuliko uwezo wangu wangu kwa sababu anatoka kwenye familia tajika," alisema.

"Ikiwa itajiri mapema, ni vizuri. Nina matumaini tu. Ninajua pia ukweli kwamba huenda ndoto yangu isitimie. Niko tayari kwa baya zaidi. "

Alisema yuko tayari kukutana na Rais Uhuru Kenyatta.