'Uhusiano wangu na Mungu ulibadilika,'Juliani afichua yaliyomtendekea baada ya kuachwa na Muigizaji Brenda Wairimu

Muhtasari
  • Juliani afichua yaliyomtendekea baada ya kuachwa na Muigizaji Brenda Wairimu
Brenda Wairimu na Juliani
Image: HIsani

Msanii JUliani amekuwa akivuma kwa muda, baada ya kufichua kwamba ni mpenziye aliyekuwa mkewe gavana wa Machakos Alfred Mutua.

Akiwa kwenye mahojiano na The Standard mapema wiki hii alifichua kwamba walikutana na Lilian Ng'ang'a JUni mwaka huu.

HUku akizungumzia uhusiano wake na mama wa mtoto wake Muigizaji Brenda Wairimu, alisema kwamba baada ya kuachwa uhusiano wake wa Mungu ulibadilika kwani alikuwa anadhani kwamba anamjua Mungu lakini hakuwa anamjua.

"Niliachwa kwa mwaka nilichafuka, nilichanganyikiwa,Lakini sasa nimetambua mimi ni nani. Uhusiano wangu na Mungu ulibadilika. Nilidhani nilikuwa na uhusiano na Mungu lakini sikuwa nayo.

Nilimwona yeye ni nani. Yeye ni mtu wa kushangaza, ananiunga mkono sana na ikiwa kutengana huko hakujatokea sikuweza kumuona vile ninavyomuona sasa.

Upendo huwa haubadiliki unapita tu," JUliani alisema.

Pia msanii huyo alimshukuru baby mama wake kwa kumshika mkono na kumruhusu amuone mtoto wao licha yao kuachana.

"Mwanzoni kulikuwa na maswala, aliondoka na hilo ni jambo zuri zaidi lililonipata.Usipotoshe.

Unapokuwa kwenye uhusiano kila wakati hudhani unafanya kile mtu mwingine anapenda lakini sio hivyo kila wakati.

Unaweza kuwa unaleta maua na yeye anaona sukuma. "