Mungu atakushangaza-Wanamitandao wamwambia Wema Sepetu baada ya kudai anamuonea Vanessa Mdee wivu

Muhtasari
  • Baada ya Vanessa Mdee na mpenzi wake Rotimi kutanganaza kwamba wamebarikiwa na mtoto mvulana, marafiki, na wanamitandao waliwapongeza

Baada ya Vanessa Mdee na mpenzi wake Rotimi kutanganaza kwamba wamebarikiwa na mtoto mvulana, marafiki, na wanamitandao waliwapongeza.

Cha kushangaza ni kuwa muigizaji wa Tanzania Wema Sepetu alisema kuwa ana wivu, lakini licha ya hayo yote alimpongeza Vanessa.

"Im sooo jealous. Congrats my baby," Aliandika Wema.

Kwa upande wake Vanessa alimshauri na kumwambia kwamba wakati wake utafika.

Pia baadhi ya wanamitandao walimtia moyo Wema Sepetu, huku wakisema siku moja Mungu atamshangaza na atakuwa na ushuuda wake.

rayhan5264: @wemasepetu soon Mungu Anaenda kukushangaza😍😍

leticiankamba: @vanessamdee Asante vee kwa kumtia moyo mwenzio...🙏🙏

saif_banker: @wemasepetu u will get in sha Allah pray to God

swai1965: @wemasepetu Dont be jealous just pray to god.

triple__hennah: @wemasepetu sooon inshallah utapata tu amini kwamba mungu yupo na wew

mily_luis0: @wemasepetu ur days are coming.. Stay patient ❤️❤️

powered_by_rich_beggars: @wemasepetu utapata nawewe kamwe usinyamanze wala usikae kimya kuongea nae, yeye niwakila mmoja wetu.

Mapema mwaka huu Wema alisema kwamba licha yake kutarajia mengi kutoka kwa mpenzi wake waliachana kwa maana hakuwa na uwezo wa kumpa mtoto.

"Kwa kweli nilikuwa nikitarajia kuolewa naye lakini jambo moja au tuseme moja ya sababu ambazo zilisababisha kuachana kwetu ni kutokuwa na uwezo wa kunipa watoto.

Ilikuwa mbaya kwangu kwa sababu kama mwanadamu, nilikuwa na matarajio yangu. na nilikuwa nikitarajia mapenzi yetu yangechipuka na kuimarishwa na ngono na mwishowe mtoto," Alisema Wema.