Mlikuwa mnataka asirudi?Nyota Ndogo awasuta wanaume wanaomkejeli kwa kurudiana na mumewe

Muhtasari
  • Nyota Ndogo awasuta wanaume wanaomkejeli kwa kurudiana na mumewe

Msanii kutoka kwenye mkoa wa pwani Nyota Ndogo,ana furaha baada ya kukutana na mumewe.

Hii ni baada ya miezi kadhaa, kuwa hawayuko pamoja na hawaongeleshani kwa utani ambao Nyota alifanya siku ya 'Fools day' mwaka huu.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram Nyota alipakia video akiwa na mumewe, wakiwa kwenye gari moshi, kisha kuandika ujumbe mfupi.

Baada ya msanii huyo kutangaza kwamba wamerudiana alipokea kejeli kutoka kwa baadhi ya wnamitandao.

Pia kuna wale walimpongeza na ata kuwatakia maisha marefu pamoja.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa isnstagram Nyota amewasuta wanaume ambao wana mkejeli, na kusema kwamba hatawapa blok bali wanapaswa kutoka kwa akaunti yake.

"WACHA NICHEKI KISENGE. Nimejaribu kupitia cooment hasilimia kubwa za comment mbaya ooh you sound desperate ooh muangalie huu mzungu ooh amefata papa.

Comment nyingi mbaya nizawanaume. Kwa papa Kwao mulisikia hakuna? Zimejaa Tele. Shida ni nini na vile hamutoki kwa hii account?

Ama mulikua hamutiki arudi? Siwezi kushangaa maana Hawa waume hawawezi Kua wanantaka mimi ama ni hasira ya kurudiwa nafeel watakua wanatamani wawe wanawake pia wasikie utamu ninaousikia mimi

Ondoka kwa account yangu KAMA hunipendi. Nafanya navyotaka hii account ni yangu. Tena mijiume mizima inatia story eti yes I this so tu

Kweli wanaume wamebaki kidogo Sana. Mimi sitawablock mutajiondoa wenyewe tu. Ila uwe tayari ukinitukana mimi nikikutukana usiniambie mambo ya kioo cha jamii hapa. Haya shururua yani Ondoka tu," Nyota aliandika.