Mama alikuwa anataka kumuuza kwa Willy Paul-Meneja wake Willy Paul afichua haya kuhusu Miss P

Muhtasari
  • Willy Paul amekuwa akishatakiwa kwa mambo kadha wa kadha na wanawake kadhaa nchini
  • Pia meneja wake alisema kwamba watu wamekuwa wakitumia jina la Willy Paul kwani ni jina kubwa nchini
Willy Paul na Miss P
Image: Hisani

Meneja wake msanii Willy Paul akiwa kwenye mahojiano amedai kwamba watu wamekuwa wakitumia jina la msanii huyo kutafuta kiki.

Willy Paul amekuwa akishatakiwa kwa mambo kadha wa kadha na wanawake kadhaa nchini.

Pia meneja wake alisema kwamba watu wamekuwa wakitumia jina la Willy Paul kwani ni jina kubwa nchini.

Alisema haya baada ya kuulizwa  kwa nini msanii huyo amekuwa akishatakiwa kila mara.

Huku akizungumzia madai ya msanii Miss P ambaye awali alidai kunyanyaswa kingono na Willy Paul alikuwa na haya ya kusema;

"Tulimchukua Miss P kama hajulikana, tuliwekeza kila kitu kwake, kumpata Miss P ilikuwa ngumu kwa maana tulitaka kujenga Brand nzuri

Willy Paul alikuwa anamtumia mamayake nauli kila siku alipokuwa anamhitaji, alisaini mkataba wa miaka 5 lakini ilikaa kwa miezi 6, siatakataa walikuwa na uhusiano wa kimapenzi, na hata mama yake alijua kwamba walikuwa katika uhusiano wa kimapenzi sio jambo la kulazimishwa

Miss P alimwambia mama yake Pozze ni mpenzi wake, mambo na pesa mama yake Miss P ndiye alianza kutisha," Alidai meneja wake Pozze.

Huku akizungumzia madai ya unyanyasaji alisema kuwa;

"Madai ya unyanyasaji ni ya uongo, baada ya mama yake kujua wana uhusiano wa kimapenzi mama yake alimlazimisha Willy Paul na shinikizo ilikuwa mingi sana

Miss P hakutaka kusikizana na Willy Paul kwani Pozze alipitisha biashara mbele,shida ilianza na Miss P kwa maana alitaka uhusiano wao uendelee lakini Pozze hakuwa anataka uhusiano huo

Katika mahojiano ambayo alifanya asilimia 90 aliyosema ni propaganda."