"Ilianza kuwa sumu!" Amber Ray aeleza kilichosababisha kutengana kwake na Jimal Rohosafi

Muhtasari

•Takriban miezi mitatu baada ya ndoa ya wawili hao igonge ukuta, Amber Ray ameweka wazi kuwa uamuzi wa kutengana kwao ulitokana  na maafikiano ya pamoja.

•Mwanasoshalaiti huyo mzaliwa wa Machakos alisema kuwa hakuna uwezekano wa kurudiana tena na mfanyibiashara huyo mashuhuri jijini Nairobi.

Image: INSTAGRAM

Mwanasoshalaiti mashuhuri Faith Makau almaarufu kama Amber Ray amefichua sababu kuu ya kutengana kwake na mfanyibiashara Jimal Marlow Rohosafi.

Takriban miezi mitatu baada ya ndoa ya wawili hao igonge ukuta, Amber Ray ameweka wazi kuwa uamuzi wa kutengana kwao ulitokana  na maafikiano ya pamoja.

Alipokuwa anashirikisha mashabiki wake kwenye kipindi cha maswali na majibu katika mtandao wa Instagram, mama huyo wa mtoto mmoja alisema  kuwa walikubaliana kutengana na Jimal miezi kadhaa iliyopita kwani ndoa yao ilikuwa imenza kuwa sumu.

"Mahusiano yalianza kuwa sumu kwa pande zetu sote wawili. Tukifaanya maafikiano ya pamoja kutengana. Hata hivyo, tuko na raha. Maisha ni ya kuishi" Amber Ray alisema.

Mwanasoshalaiti huyo mzaliwa wa Machakos alisema kuwa hakuna uwezekano wa kurudiana tena na mfanyibiashara huyo mashuhuri jijini Nairobi.

"Tutapatana tena siku ya mwisho mbinguni" Amber Ray alimjibu shabiki aliyetaka kujua wakati anakusudia kupatana tena na Jimal.

Hata hivyo Amber Ray alisema kuwa bado anatazamia kuwa kwa ndoa siku za usoni kwani bado anaamini kuwa kuna mapenzi ila hatakubali kuwa kwenye mahusiano sumu.

"Naamini kuna mapenzi na ndoa, lakini tena yakiwa sumu kwangu hayafai" Alisema Amber Ray.

Mwanasholaiti huyo pia alifichua kuwa alipata mtoto wake wa kwanza, Garvin akiwa na umri wa miaka 19 tu. Hata hivo mahusiano kati yake na baba ya mwanawe hayakudumu kwa wakati mrefu.

Kwa sasa Jimal amerudiana na mke wake Amira ambaye walitofautiana sana kufuatia uamuzi wake wa kumuoa Amber Ray kama mke wa pili.

Wawili hao tayari wamerejesha uhusiano mzuri kati yao huku wakionekana wakisherehekeana mitandaoni mara kwa mara.