'Churchill hana deni la mtu,'Eric Omondi awaonya wachekeshaji wanaomsuta Mwalimu Churchill

Muhtasari
  • Eric Omondi awaonya wachekeshaji wanaomsuta Mwalimu Churchill
Eric Omondi

Mchekeshaji Eric Omondi amewapa wachekeshaji wenzake onyo, kwa kumshambulia mmiliki wa kipindi cha churchill Mwalimu Churchill.

Huku akijitambulisha kama kifungua mimba wa Chuchill katika tasnia ya burudani, amesema kwamba amechoka kusikia watu wakimkejeli na kumshambulia Churchill.

Eric amewaambia atakaposikia maneno mabaya dhidi ya Chuchill kwa ahakika hata laza damu kwani atakabiliana nao ipasavyo.

Aidha ameweka wazi kwamba Curchill hana ddeni la mtu, na wachekeshaji ambao wamekuzwa na Mwalimu wanapaswa kumjengea nyumba kama ishara ya kumshukuru.

"Kama mtoto wa kwanza wa @mwalimchurchill sitaki kamwe kusikia,mchekeshaji mwingi akiongea mbaya kuhusuCHURCHILL.

Nikiskia Mjinga mwingine tena akisema ati Churchill "alinitumia"...Ntakuja personally na nikupige mangumi za Uso na Tumbo.

Churchill hana deni la mtu😡😡😡😡😡kama kuna kitu wachekeshaji wote ambao walipitia mikononi mwa Churchill wanapaswa kuja pamoja na kumjengea nyumba Machakos PUGAA!!!," Alisema.

Kama tunavyojua Eric anapenda kutafuta kiki kutoka kwa mashabiki, lakini je kamahatafuti kiki ana zungumzia mchekshaji yupi na kwa nini?