Kwa nini maisha ya Juliani yawe hatarini?-Lilian Ng'ang'a amuuliza Mike Sonko

Muhtasari
  • Lilian Ng'ang'a ajibu ujumbe wake Sonko  kuwa anahatarisha maisha ya juliania anahatarisha maisha ya juliani
Lilian Ng'ang'a na Juliani
Image: Boniface Mwangi/Twitter

Kwa muda sasa JUliani na Lilian Ng'ang'a wamekuwa wakigonga vichwa vya habari, baada ya wawili hao kutangaza kwamba wao ni wapenzi.

Picha za wawili hao zilizopakiwa na mwanaharakati Boniface Mwangi ziliibua mdahalo mitandaoni JUmapili asubuhi.

Mwangi aliwashauri wanamitandao kwamba wanapaswa kuenda mahali wanpendwa na wala sio kukaa kwenye uhusiano wenye vurugu kwa ajili ya dini au jamii.

Wakati huo huo aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko alipakia picha hizo kwenye ukurasa wake wa facebook, na kumshauri Lilian aendelee na maisha kwa amani.

Pia sonko alidai kwamba maisha ya msanii JUliani yanaweza kuwa hatarini kwa ajili yake.

Huku akijibu madai hayo LIlian alimuuliza Sonko kwa nini maisha ya mpenzi wake yawe hatarini, kwa ajili yake.

Aidha Lilian ameweka wazi kwamba picha hizo hazikuwa kwa njia yeyote muumiza mtu yeyote, huku akisema kwamba jamii inapaswa kuwa sawa kwa wanawake.

"Wasiwasi wangu kuu kutoka kwa chapisho la Gavana Mike Sonko ni KWANINI angedhani ninahatarisha maisha ya Juliani. Picha zilizoshirikiwa jana na rafiki yetu Bonnie hazikuwa kwa njia yoyote ile iliyokusudiwa kumuumiza mtu yeyote.

Je! Maoni yangekuwa sawa ikiwa mwanamumendite ambaye sasa alikuwa akichumbiana na mtu mwingine? Nina hakika kwa 100% isingekuwa.

Jamii LAZIMA iwe sawa kwa wanawake.Pia,Ukisoma chapisho hili na usione LITU KUU linalohitaji mazungumzo, unashindwa dada zako, binti zako, marafiki wako wa kike nakadhalika," Lilian anasema.

Je drama ii itaendelea mpaka lini?