BARAKA YA MASHUJAA DAY!

Hongera! Mwanasoshalaiti Vera Sidika ajifungua mtoto wa kike, Asia Brown

Muhtasari

• Vera ametangaza kwamba alijifungua mtoto msichana mwendo wa saa nne na dakika ishirini na moja asubuhi ya Jumatano

•Mwanasoshalaiti huyo mwenye umri wa miaka 31  alijifungua kwa njia ya upasuaji almarufu kama CS kama  alivyokuwa anataka

Image: INSTAGRAM// VERA SIDIKA

Hatimaye mwanasoshalaiti  mashuhuri nchini Vera Sidika na mpenzi wake Brown Mauzo wamemkaribisha kifungua mimba wao.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Vera ametangaza kwamba alijifungua mtoto msichana mwendo wa saa nne na dakika ishirini na moja asubuhi ya Jumatano.

Vera aliambatanisha tangazo lake na picha iliyoonyesha wakiwa na mumewe kwenye chumba kilichoonekana kuwa wadi huku mtoto wao akiwa amelazwa kwa kitanda cha mtoto kilichokuwa kando. Wawili hao walionekana wenye bashasha tele.

Alipokuwa anatangaza habari kuhusu kujifungua kwake, Vera alisema kwamba binti yao ataishi kuwa miujuza ambayo itakamilisha maisha yake na mumewe mwanamuziki Brown Mauzo.

"Tarehe 20.10.2021 mida ya saa nne na dakika 21 asubuhi, mtoto wa malkia alizaliwa. Asia Brown @princess_asiabrown. Utaishi kuwa miujiza ambayo itafanya maisha yetu yawe kamili" Vera alitangaza.

Mauzo kwa upande wake alimshukuru Mungu kwa baraka ya mtoto.

Mamia ya mashabiki wa wanandoa hao wamefurika mitandaoni kuwapongeza kufuatia baraka hiyo  iliyowafikia siku ya Mashujaa Day.

Mwanasoshalaiti huyo mwenye umri wa miaka 31  alijifungua kwa njia ya upasuaji almarufu kama CS kama  ilivyokuwa mapenzi yake

Hapo awali Vera  alikuwa ameeleza kwamba angependa kujifungua kwa njia ya upasuaji kwani anaogopa sana uchungu wa leba.

Wapenzi hao wawili wamempatia binti yao jina Asia Brown na tayari wamemfungulia ukurasa wa Instagram @princess_asiabrown.

Kutoka Radio Jambo tunamtakia Asia Brown maisha mema!