Mama yangu anachukia sana kila nikimwambia sitaoa-Burna Boy afunguka

Muhtasari
  • Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram,msanii huyo alisema kwamba mama yake anachukia sana endapo anamwambia kwamba hatawahi oa
Burna Boy
Image: Hisani

Msanii maarufu kutoka Nigeria Burna Boy amefunguka na kufichua jinsi mama yake huchukia wazo lake la kutooa.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram,msanii huyo alisema kwamba mama yake anachukia sana endapo anamwambia kwamba hatawahi oa.

“Mama yangu anachukia sana kila nikimwambia sitaoa anabadilika na kuwa mwekundu, suala langu mwenyewe ni kwamba sasa nina uhakika sana kama ninamaanisha kweli au niseme tu ili kumkasirisha," Aliandika Burna boy.

Ndoa ni jambo ambalo wengi hutamani, huku baadhi ya watu wengi wakichagua chaguo lao kwa ajili ya shinikizo kutoka kwa marafiki na familia.

Kile wengi hawafahamu au vijana wa karne hii hawajui ni kwamba ndoa ni jambo la maisha na kila mtu anapaswa kuwa makini akianya chagu lake.

Awali uvumi ulienea sana kwamba Burna Boy na Stefflon Don ni wachumba.