Ali Kiba asimulia alivyonusurika kubakwa na wanadada watatu

Muhtasari

•Mwanamuziki huyo ambaye amekuwa akivuma kwa kipindi cha zaidi ya mwongo mmoja alieleza kuwa tukio hilo lilitokea baada ya rafiki yake kusahau kufunga mlango wa chumba alichokuwa analala.

Image: INSTAGRAM// ALI KIBA

Nyota wa muziki Ally Saleh Kiba almaarufu kama Ali Kiba amekiri kuwa amewahi nusurika kubakwa na wanadada kwa wakati mmoja. 

Akiwa kwenye mahojiano na Bi Salama Jabir hivi karibuni, staa huyo wa Bongo alisimulia alivyonusurika kubakwa na wanadada watatu baada ya kumaliza kutumbuiza katika tamasha iliyofanyika nchini Marekani.

Mwanamuziki huyo ambaye amekuwa akivuma kwa kipindi cha zaidi ya mwongo mmoja alieleza kuwa tukio hilo lilitokea baada ya rafiki yake kusahau kufunga mlango wa chumba alichokuwa analala.

"Nilinusurika kubakwa. Hilo ni mbaya sana kusema.Kuna kipindi fulanu ambapo nilienda kufanya shoo. Kule kulikuwa na kikomo cha kukaa kwa muda fulani kwa hivyo tukawa tumetoka. Shoo ikiisha wanafanya sherehe ya baada ya tamasha. Tulikuwa tunachukua  chumba kimoja kikubwa cha hoteli ili kufanyia sherehe. Kama tumechukua vyumba nane tumechukua tulikuwa tunaongeza chumba cha tisa cha kufanyia sherehe ya baada ya tamasha. Hicho chumba cha tisa ndicho kilikuwa na sherehe.

Tulipokuwa tunafanya sherehe ikafika muda fulani nikawa nimechoka nikataka kulala. Nikaenda kulala hata bila kuwaaga pale kwa sababu lazima kuna watu walikuwa wananiangalia pale. Nakumbuka tukio hilo vizuri ilikuwa hivo. Nilitoka kwenye chumba cha sherehe nikaenda kwa chumba ambacho nilikuwa nalala. Nikatafutwa pale kwa sherehe nami sipatikani.  Walikuwa wanauliza nilienda wapi. Walikuwa wananiita mtoto, eti mtoto kaenda wapi jamani?

Brasa akaja kunitafuta kwa chumba changu akaniambia eti walikuwa wananitafuta. Akaniambia 'tunakutafuta kumbe umekuwa ukilala, si ungesema unataka kulala basi tukuache.  Ulikuwa umetutisha, ulikuwa umetutia wasiwasi tusijue ni namna gani.' Mimi nikamwambia ni sawa akatoka akasahau kufunga mlango.

Wale mademu wakaulizia Ali ako katika chumba kigani. Wakatajiwa chumba changu wakaja mademu watatu" Alisimulia Ali.

Hata hivyo alisema kwamba alinusurika kutoka kwa tukio hilo.