Hamtatutoa figo hapa na mambo ya familia,'Akothee awatetea Kabi Wajesus na Milly Wajesus

Muhtasari
  • Milly na Kabi walisafiri hadi Dubai na baadaye wakaenda Uturuki waliko sasa hivi
  • Kupiga picha na mtoto wako kwenye picha haimaanishi kuwa wewe ni mzazi mzuri
Image: INSTAGRAM// KABI WA JESUS

Akothee ni mmoja wa watu mashuhuri kwenye mitandao ya kijamii na mtu mashuhuri ambaye anaishi maisha ya kifahari yanayoonekana katika machapisho yake ya Instagram.

Kwa upande mwingine familia ya Wajesus inayojumuisha Kabi, Milly na mwana wao Taji ni waundaji wa maudhui wanaojulikana ambao wanamiliki chaneli maarufu ya YouTube na duka la nguo lililopewa jina la Bossman.

Mapema wiki hii Milly na Kabi,walifichuliwa na mwanablogu Edgar Obare kwa kuto mtunza na kumlea mtoto wao vyema.

Milly na Kabi walisafiri hadi Dubai na baadaye wakaenda Uturuki waliko sasa hivi.

Kwenye moja ya machapisho ya Edgar, shabiki ambaye hajatambuliwa alisema kuwa Wajesus hawampi mtoto wao matunzo muhimu ya wazazi.

Aliendelea na kufichua kuwa pia wamekataa kumtunza mtoto wao wa kambo Abi. Walakini, familia hii hadi sasa haijazungumzia suala hili.

Watu kadhaa mashuhuri akiwemo Sarah Kabu Mkurugenzi Mtendaji wa Bonfire Adventures walikuja kujitetea na kuwaambia watu waepuke kumhukumu Milly.

Akothee pia kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram kuwashauri watu jinsi ya kulea watoto wao.

Aliwataka watu kuelewa kuwa Wajesus ni familia changa tu na haiwezi kuendelea kutembea na mtoto.

Kupiga picha na mtoto wako kwenye picha haimaanishi kuwa wewe ni mzazi mzuri.

Huu hapa ujumbe wake Akothee;

Kila mtu alee mtoto wake vile anajua . Angalau kabis wana timu inayosaidia ambayo inawasaidia kutunza mtoto wao wakati wanatafuta riziki

Ikiwa wangevunja sheria leo na kutuma bili ,mtawatukana, saa hii ,wanajaribu kutafuta maisha kando na umaarufu ,unataka kuwafanya wajisikie kama wazazi wasiowajibika

Kwa sababu tu umesahau kuchambua maisha yako mwenyewe na amka tu kufuata kile ambacho watu mashuhuri wana pakia! 🤔 Ala!

Hatutakubali kudhulumiwa pia nasi tuna maisha baada ya kamera Unapaswa pia kutuonyesha jinsi unavyowatunza watoto wako ili tukunakili 🤔! Tuna wazazi ambao wanakuwepo majumbani mwao kuanzia Jumatatu hadi Jumatatu, lakini hawapo katika Maisha ya watoto na kuwatunza.

Kabi na milly ni wanandoa wachanga, pia wanahitaji muda wa mimi na hawawezi kumbeba mtoto kila mahali kwa ajili ya kukufurahisha wewe au mitandao ya kijamii."