Harusi tunayo, hatuna? Dalili zinazoashiria huenda Larry Madowo hatimaye amepata kipenzi cha maisha yake

Muhtasari

•Uvumi umetanda baada ya Madowo na Bi Kimani kupakia picha zilizoonyesha wakiwa kwenye kipindi kizuri pamoja  na kuziambatanisha na jumbe tamu za mapenzi.

•Picha ambayo Madowo alikuwa amepakia mwaka wa 2014 wakiwa wanakula na kunywa pamoja na Edith katika hoteli ya Kenchic ilifukuliwa na baadhi ya wanamitandao. 

•Maelfu ya Wakenya wamekuwa wakishangaa lini mtangazaji huyo gwiji mwenye umri wa miaka 34 atafunga ndoa huku wengi wakitazamia kuona mwanamke atakayeyeyusha moyo wake.

Image: INSTAGRAM// LARRY MADOWO

Wikendi iliyotamatika mwandishi wa habari mashuhuri Larry Madowo  na malkia anayetambulika kama Edith Kimani wamezungumziwa sana mitandaoni.

 Hii ni baada yao kupakia picha zilizoonyesha wakiwa kwenye kipindi kizuri pamoja  na kuziambatanisha na jumbe tamu za mapenzi.

Wawili hao waliitana majina matamu ya mapenzi na kuibua dhana miongoni mwa wanamitandao kuwa huenda ni kweli wanachumbiana.

"My sweet @larrymadowo" Bi Kimani aliandika chini ya picha yao ambayo alipakia huku Madowo akimjibu "Hey boo!" 

Matendo ya wawili hao ya hivi karibuni kwenye mtandao wa Instagram yameibua gumzo kwamba huenda wameamua kuweka mahusiano yao hadharani.

Imebainika kwamba sio mara ya kwanza wawili hao kuonekana pamoja.

Picha ambayo Madowo alikuwa amepakia mwaka wa 2014 wakiwa wanakula na kunywa pamoja na Edith katika hoteli ya Kenchic ilifukuliwa na baadhi ya wanamitandao. 

"Tulienda date yetu ya pili na Edith katika hoteli ya Kenchic na akalipia tena" Madowo aliandika chini ya picha hiyo.

Picha hiyo kutoka miaka saba iliyopita imewafanya wengi kuamini kuwa Madowo na bi Kimani wamekuwa kwenye mahusiano kwa kipindi kirefu ila bado hawajadhihirisha wazi kuwa wanachumbiana.

Ingawa haijabainika wazi kama kwa kweli wanachumbiana ama ni urafiki wa kawaida tu, baadhi ya wanamitandao ikiwemo watu mashuhuri wamejitokeza kuwapongeza wawili hao huku wengi wakikadiria kuwa huenda watafunga ndoa hivi karibuni.

@eddiebutita nimekuwa najiuliza pilau nakula wapi hii mwaka

@bettymuteikyallo Alililii

@sharon_momanyi Harusiiiii!

@marie.zihy nani mwingine anatumai kuwa ni ukweli

Maelfu ya Wakenya wamekuwa wakishangaa lini mtangazaji huyo gwiji mwenye umri wa miaka 34 atafunga ndoa huku wengi wakitazamia kuona mwanamke atakayeyeyusha moyo wake.

Hayawi hayawi basi huwa, matukio ya wikendi ni dalili kubwa kuwa huenda hatimaye siku hiyo imetimia.