"Utatumiwa kisha uachwe!" Shakilla amuonya Miss P kufuatia madai kuwa alipachikwa ujauzito na Eric Omondi

Muhtasari

•Shakilla amedai kwamba pia yeye aliwahi kudanganya kuwa alipachikwa ujauzito na Eric Omondi.

•Ametahadharisha Miss P kwamba nia ya mcheshi huyo na kumtumia tu kutafuta kiki na baada ya hayo atatemwa tu jinsi yeye na wengine waliwahi kutemwa pia.

Image: INSTAGRAM

Mwanasoshalaiti maarufu kwenye mitandao ya kijamii anayetambulika kama Shakilla amejitokeza kufutilia mbali ujauzito wa mwanamuziki Miss P.

Siku ya Jumatatu mcheshi Eric Omondi alidai kwamba alimpachika Miss P ujauzito walipopatana miezi mitano iliyopita.

Hata hivyo, Shakilla amepuuzilia mbali madai hayo huku akiwashutumu wasanii hao wawili kuwa wanadanganya kuhusu ujauzito huo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Shakilla amedai kwamba pia yeye aliwahi danganya kuwa alipachikwa ujauzito na Eric Omondi.

"Mwanzoni ilikuwa mimi ambaye niliyedanganya kuwa na ujauzito wa binti yao. Baada ya majaribio mengi ya kupata video nzuri, tena naona picha nyingine iliyokarabatiwa vibaya ya msichana mwingine asiyejua akidai kwamba ataolewa. Wakati mwingine ili kupata matokeo mazuri mjaribu kuagiza angalau tumbo ghushi ama mtafute huduma za mkarabati picha mzuri" Shakilla alisema.

Mwanasoshalaiti huyo ambaye kwa wakati mmoja alidai aliwahi kulala na  baadhi ya watu mashuhuri kama Victor Wanyama, Willy Paul na Khaligraph Jones pia amefutilia mbali madai ya Omondi kwamba atakuwa baba mwenye kuwajibika.

Ametahadharisha Miss P kwamba nia ya mcheshi huyo na kumtumia tu kutafuta kiki na baada ya hayo atatemwa tu jinsi yeye na wengine waliwahi kutemwa pia.

"Eti uwajibikaji, upuzi tu. Mwambie ajifunze kutoka kwa wengine. Atatumiwa na aachwe baada yao kupata watazamaji" Alisema Shakilla.

Kwenye mtandao wa Instagram Omondi na Miss P walipakia picha iliyomuonyesha mpenzi huyo wa zamani wa Willy Paul akiwa mjamzito huku Omondi akiwa amemshika tumboni.

Omondi alidai kwamba walipatana na Miss P miezi mitano iliyopita katika tamasha ambayo alikuwa anafanya na baada ya hapo tamasha wakaamua kushiriki mchezo wa kitandani pamoja.

Mcheshi huyo alisema kuwa tayari alimhakikishia Miss P kuwa atawajibikia mtoto aliyebeba huku akidai kuwa watoto ni baraka kutoka kwa Mungu.

"Nilipatana na mwanamke huyu mrembo miezi tano iliyopita  katika tamasha ambayo nilikuwa nafanya. Kilichotendeka kilitendeka na nilimuahidi kuwa nitawajibika. Watoto ni baraka kutoka kwa Mungu" Omondi aliadika kwenye ukurasa wake wa Instagram.