Hawa wazungu wako wapi-Akothee ajibu madai kwamba anawauza wasichana wadogo kwa wazungu

Muhtasari
  • Akothee ajibu madai kwamba anawauza wasichana wadogo kwa wazungu
Image: INSTAGRAM// AKOTHEE

Msanii Esther Akoth almaarufu Akothee ​​kupitia kwenye uurasa wake wa instagram amejitokeza wazi kujibu madai kwamba yeye huwasafirisha wasichana wadogo kwa wazungu kwa malipo na hii ni mojawapo ya vyanzo vyake vya utajiri wake.

Mwanablogu mmoja kwa jina Makiadi  kwenye ukurasa wake wa Instagram alihoji umma na wanamitandao ikiwa wanajua chanzo kikuu cha mapato cha mwimbaji Esther Akoth ambaye kwa kawaida hujulikana kama Akothee.

Aliendelea kutaja kwamba Akothee ​​huwasafirisha wasichana wadogo ili waolewe na Wamarekani wazee kwa kubadilishana pesa.

Madai na uvumi huu ulizua mazungumzo mengi mitandaoni kwani baadhi ya wanawake wengine walikuwa tayari kuhusishwa na tajiri Wazungu kama inavyodaiwa.

Walitamani hata wapewe fursa sawa ili waweze kubadilisha hali yao ya kifedha.

Hata hivyo, wakati akijibu madai hayo, Akothee alianza kwa kusema kuwa wakati watu hawawezi kukufafanua kauli ambayo aliendelea na emoji ya kucheka.

Aliendelea kusema kuwa madai hayo yalikuwa makali kwake, hata hivyo, aliongeza kuwa pia anahitaji kujisafirisha akidai kuwa pia amechoka kulipa bili zake.

"Wakati hawawezi kukufafanua,Hii ni kali ,nataka kujiuza pia nimechoka kulipa bills haki ,Hawa wazungu wako wapi," Akothee alisema.