Wakati huo nilikuwa namchumbia mke wangu,'Sam Ogina akanusha madai ya kumchumbia Jacque Maribe 2012

Muhtasari
  • Mwanahabari huyo alisema wakati huo alikuwa akimchumbia mke wake wa sasa, Priscathi Njeri Oguna
Image: Twitter/Sam Ogina

Mwanahabari wa runinga ya Citizen  Sam Ogina amekanusha madai kwamba alichumbiana na Jacque Maribe mwaka wa 2012.

Kauli yake ilijiri saa chache baada ya mcheshi Eric Omondi kumtaja Ogina akidai kuwa wakati alipokutana na Maribe, wawili hao (Maribe na Ogina) walikuwa katika uhusiano wa kimapenzi.

Eric alikuwa akijitetea kutokana na madai kuwa yeyehawajibikiimahitaji ya mwanawe na kuongeza kuwa amekuwa akitaka uchunguzi wa DNA ili kuthibitisha kuwa yeye ndiye baba wa mtoto wa Jacque.

Akijibu madai hayo, Sam Ogina alikanusha vikali madai hayo na kutishia kufichua Eric ambaye anasema alitaka kuchumbiana na mkewe Njeri.

Mwanahabari huyo alisema wakati huo alikuwa akimchumbia mke wake wa sasa, Priscathi Njeri Oguna.

"Mimi Sam Ogina ningependa kukanusha kabisa madai ya Eric Omondi kwamba nilikuwa nachumbiana na Maribe 2012

Alichochapisha ni uwongo na kashfa na acha awe na uhakika kwamba ninamjia. Wakati huo nilikuwa nachumbiana na mke wangu kipenzi Njeri," Aliandika Sam.

Ogina zaidi aliamuru kwamba Eric afute chapisho hilo kutoka kwa mtandao wake wa kijamii na kuomba msamaha mara moja bila masharti.