Wamerudiana ila yeye ndiye 'sidechick'-Mange Kimambi adai Rayvanny na Fayvanny wamerudiana

Muhtasari
  • Mange Kimambi adai Rayvanny na Fayvanny wamerudiana

Mwanaharakati wa Tanzania Mange Kimambi kupitia kwenye ukutasa wake wa instagram amefichua maisha ya mapenzi ya staa wa bongo Rayvanny.

Kulingana na Mange wawiili hao walikuwa kwenye hoteli, wakionyeshana mapenzi, na kudai kwamba Paula ndiye mpenziwe Rayvanny, na Fayvanny amekuwa mpango wa kando.

"Leo lunchtime walikuwa pamoja Havanna. Wakakaa VIP mabusu kama yote. Mapenzi kama yooote.mahaba kama yooote.

Kwa kifupi wamerudiana Ila Fayhma kapewa down grade from main to side chick. Yani yeye now ndo anafichwa Paula ndo main," Alisema Mange.

Aidha amefichua kwamba hoteli ambayo msanii huyo alidai ni yake, sio yake bali ni ya Mkenya, ambaye wanatumia jina lake kuikuza.

"By the way na hiyo Havana sio ya RayVanny ni ya Mkenya. Yeye analipwa ili watumie jina lake kuikuza. Hana hata share moja

WaKenya wana akili, wametujua watanzania watu wa Kiki so nao wanafungua biashara wanatugea vihela vidogo then wanatembea na kiki za wabongo 🤣🤣🤣🤣Msiniulize nimeitoa wapi? Mkiniuliza sana mpaka owner kamili wa Havanna ntamtaja kwa majina kamili.."