"Hakuna aliyenichukulia kama mtu mgonjwa" Vera Sidika azungumza kuhusu afya yake baada ya upasuaji

Vera amesema upasuaji ambao alifanyiwa haukumwathiri kwa namna yoyote.

Muhtasari

•Mpenzi huyo wa mwanamuziki Brown Mauzo amedai kwamba hakuhisi uchungu wowote alipofanyiwa upasuaji na hata baada ya kujifungua.

•Amesema kwamba baada ya kufanyiwa upasuaji hakuna yeyote aliyemchukulia kama mgonjwa kwa kuwa hakuwa na maumivu yoyote.

•Wiki chache zilizopita, mama huyo wa mtoto mmoja aliwasuta waliokuwa wanamuombea maovu huku akiwaarifu kwamba yeye pamoja na bintiye wako hai na wanaendelea vyema.

Image: INSTAGRAM// VERA SIDIKA

Mwanasoshalaiti Vera Sidika amesifia sana chaguo la kujifungua kupitia njia ya upasuaji.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Vera ambaye alijifungua mtoto wake wa kwanza kwa njia ya upasuaji takriban wiki tatu zilizopita amesema kwa sasa mbinu za upasuaji wa ujauzito almaarufu kama CS zimeendelea na kuboreshwa sana.

Mpenzi huyo wa mwanamuziki Brown Mauzo amedai kwamba hakuhisi uchungu wowote alipofanyiwa upasuaji na hata baada ya kujifungua.

"Nilisema sijahisi uchungu wowote tangu nilipofanyiwa upasuaji hadi wa leo lakini watu hawaniamini kwa sababu wamezoea mbinu mzee za CS ambazo kila mtu aliogopa. Tena wanadhani eti sote tunaenda kwa daktari na hospitali moja kwa hivyo wanatarajia uhisi uchungu kama wa waliohisi" Vera amesema.

Mwanasoshalaiti huyo mwenye umri wa miaka 32 amesema upasuaji ambao alifanyiwa haukumwathiri kwa namna yoyote.

Amesema kwamba baada ya kufanyiwa upasuaji hakuna yeyote aliyemchukulia kama mgonjwa kwa kuwa hakuwa na maumivu yoyote.

"Hakuna aliyenichukulia kama mgonjwa baada ya CS kwa kuwa nilikuwa tu kama kawaida yangu. Kwa wakati mwingine huwa natamani ningefanya kuwa mgonjwa ama nahisi uchungu ili nipewe huduma zaidi kama mtu mgonjwa na nihurumiwe... Nikiwa hospitalini nilikuwa napewa dawa za kutuliza uchungu  zenye nguvu kila wakati kwa hivyo sikuhisi uchungu wowote. Hata niliweza kukaa chini kwa kitanda cha hospitali masaa machache baada ya upasuaji. Sikula chochote baada ya masaa 6-7. Nilichohisi ni kiu na walipunguza kiasi cha maji ambacho nilifaa kunywa" Alisema Vera.

Wiki chache zilizopita, mama huyo wa mtoto mmoja aliwasuta waliokuwa wanamuombea maovu huku akiwaarifu kwamba yeye pamoja na bintiye wako hai na wanaendelea vyema.

"Nashukuru sana kwa maombi yenu. Nilifanikwa kufanyiwa upasuaji salama na nikajifungua Asia. Mimi na mtoto tuko salama na wazima. Tunashukuru Mungu" Alisema Vera.

Vera alisema mtoto wake ni kila kitu alichowahi kutamani maishani huku akieleza alitengenezwa kwa mapenzi ya dhati  siku ya wapendanao ya Valentine's.

"Asia Brown, kila kitu ambacho niliwahi kutamani. Mtoto wetu alitengenezwa kwa mapenzi ya dhati siku ya Valentines. Ni mrembo sana. Mtoto mrembo zaidi ambaye nimewahi kuona. Mungu ni muumba kweli" Vera alisema.