Nilirudisha gari kwa muuzaji,'Vitu ambavyo Lilian Ng'ang'a alikaata kutoka kwa Alfred Mutua

Muhtasari
  • Pia alipendekeza kumuoa kupitia harusi  lakini bado alikataa matamanio yake
Aliyekuwa mpenzi wa gavana Mutua Lilian Ng'ang'a
Aliyekuwa mpenzi wa gavana Mutua Lilian Ng'ang'a
Image: MERCY MUMO

Lillian Nganga amefichua kwamba Gavana Alfred Mutua alijaribu sana kumrejesha baada ya kutengana miezi michache iliyopita.

Mkewe  wa zamani wa gavana wa Kaunti ya Machakos alisema kuwa Mutua alimnunulia gari jipya mnamo Septemba ambalo alimrudishia mchuuzi.

Mutua pia alijitolea kumnunulia nyumba ya kifahari na kumsaidia kifedha lakini bado alikataa kwa vile alikuwa tayari ameamua.

Pia alipendekeza kumuoa kupitia harusi  lakini bado alikataa matamanio yake.

Akijibu wale wanaomshutumu kwa kumpenda Gavana kwa sababu ya faida za kifedha, aliandika;

"Na kwa wale wote ambao mstari wao pekee wa mashambulizi ni vitu vya kimwili, Alfred alininunulia gari jipya miezi 2 iliyopita. Niliirudisha kwa muuzaji. Alijitolea kuninunulia nyumba mpya, kunifadhili kifedha, kunitafutia kazi nk nilikataa. Alitaka tuoane kwa harysi. Nilikataa," Aliandika Lilian.

Huku wawili hao wakionekana kuwa na uhusiano mbaya katika kipindi cha miezi michache iliyopita, Lilian amedai kuwa mapenzi yake ni watengane vizuri kama watu wazima.

Kupitia ujumbe ambao alichapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram asubuhi ya Jumapili, Lilian amesema angependa kuwe na amani kati yake na gavana Mutua ila sio kisasi.

"Mimi ningependa tuwe na utengano mzima na wenye urafiki. Ningependa amani kati yetu na mwishowe tuwe marafiki, baada ya yote tumekuwa pamoja kwa mwongo mmoja" Lilian alisema.