Aliniambia nitume picha nikiwa uchi,'Shorn Arwa awashauri wasanii wa kike nchini

Muhtasari
  • Shorn Arwa awashauri wasanii wa kike nchinira
  • Shorn alisema kwamba alimwambia kiini cha kumtumia picha akiwa uchi ni ili watafute kiki
Shorn Arwa
Image: Studio

Muunda maudhui Shorn Arwa ambaye alifahamika sana mwaka jana baada ya kuigiza, mchezo unaouhusiana na kisasi cha sasa haswa wanawake, kupitia kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii amefichua kwa nini hajakuwa akifanya kazi na wasanii wengine.

Kulingana na Shorn, kupitia kwa video aliopakia, alisema kwamba msanii mmoja nchini ambaye anafahamika sana nchini, alimshauri amtumie picha zake akiwa uchi.

Shorn alisema kwamba alimwambia kiini cha kumtumia picha akiwa uchi ni ili watafute kiki.

Shorn amekuwa akiigiza na wasanii tofauti miongoni mwao ni mcheshi Mammito, ambaye anafahamika sana kupitia uchekeshaji wake.

"Nimekumbuka kitu ambacho mtu aliniuliza mbona sifanyi kazi na wasanii, awali kuna mtu ambaye anafahamika sana aliniambia kuwa kwenye mitandao ya kijamii naonekana nikiwa mkali sana na kuwa katika maisha ya kawaida mimi sio mkali

Kwa ivyo aliniuliza ama anaweza 'take risk' nilimwambia kama ni mambo na pesa naweza, yaani alifungua mdomo wake na kuniuliza kwa mfano, kama leo nikwambie utume picha ukiwa uchi ili tutafute kiki utakubali

Nilishangaa sana nikamuuliza kwa hivyo ndio huwa mnawafanyia wasichana na pia wasanii wa kike chipukizi na kisha mnawaacha

Ni wazimu kwa maana sielewi kwa nini ufanye kiki kama hiyo heri nikae kwetu,aliniambia haiewezi kama huwezi onyesha nyama siwezi kula nyama

KIle nilikuwa najaribu kusema ni kuwa kama wewe ni mwanamkke kama mimi, haustahili kufanya mambo mabaya, kwa sababu ya kiki

Wataona uch wako, watazungumza kwa wiki lakini mitandao ya kijamii haitajua ulikuwa unatafuta kiki, baada ya kupata kile walikuwa wanataka watakuacha

Mitandao haitajua kwamba ulikuwa umeambiwa ufanye hayo, fanya kazi kwa bidii na muachane na hawa wajinga," Shorn alisema.