Sina roho mbaya-Otile Brown asema huku akiwakashifu Mbosso na Zuchu

Muhtasari
  • Otile Brown awaambia Mbosso na Zuchu waache mazoea

Msanii Otile Brown amewakshifu wasanii wa lebo ya Wasafi Zuchu na Mbosso kwa kutumia mistari ya kibao chake kwenye wimbo wao mpya.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram Otile amewauliza wasanii hao wawili waache mazoea, ila hana roho mbaya.

"Punguzeni mazoea basi … Hio ni melody nzima ya baby love , if you know you know .. mnabahati sina utoto na roho mbaya .. anyways ❤️ link in their bio #justinlovemusic #wegotnothingbutlove," Aliandika Otile.

Hizi hapa baadhi ya hisia za mashabiki baada ya ujumbe wake Otile Brown;

yycomedian: Kwanza hapo kwa kwenye giza giza totoro...jiko jiko langu

eddy_ste.veIvo Ivo:  twatambua Otile sisi,,

brandon_brandy_officialLegend: ushazungumza👏🔥

supgizzoglikizo: Wamezidisha sio sili🔥🔥

_itskaleogodwin: Whaaa wakenya mliamua November ikue tu chaos😂🙌