'Sijawahi kuwa kwenye mahusiano na mwanamke!' Mke wa Bien ajibu madai kuwa alicheza karata nje na Makena Kimathi

Muhtasari

•Chiki amepuuzilia mbali madai ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi na aidha Michelle ama Makena huku akieleza hajawahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamke mwenzake

Image: INSTAGRAM// CHIKI KURUKA

Chiki Kuruka ambaye ni mke wa mwanamuziki Bien wa bendi ya Sauti Sol amezungumzia madai kuwa ndiye sababu ya kutengana kwa Michelle Ntalami na Makena Njeri.

Kupitia mtandao wa Instagram, Chiki amepuuzilia mbali madai ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi na aidha Michelle ama Makena huku akieleza hajawahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamke mwenzake.

Chiki alikuwa anajibu shabiki mmoja aliyetaka kujua sababu uliza sababu zake za kutenganisha wapenzi hao wawili.

"Mbona ulitenganisha Michelle na Makena" Mtumizi wa Instagram aliuliza.

Chiki alisema ingawa anaunga mkono na kuheshimu mahusiano kati ya watu wa jinsia moja, yeye mwenyewe  hajawahi jihusisha na mahusiano kama yale.

Kwa kawaida ningepuuza haya. Lakini nadhani nina wakati sasa hivi. Tufanye hivi tuwatag watu unaozungumzia maana ninavyofahamu @michelle.ntalami hajawahi kutaja jina langu kwenye jumbe zake. Sijawahi kuwa na uhusiano na mwanamke. Badala yake daima nimetoa msaada wangu kwa jamii ambayo ninaipenda na kuiheshimu sana. Lakini hawa wanaosisitiza wanaanza kunikasirisha, si kwa sababu wakwe zangu wanapaswa kujibu haya, lakini kwa sababu wanadamu kama WEWE hukataza washirika kusema. Siku zote sikuwa na chochote kingine isipokuwa heshima kwa Michelle kwa kweli. Lakini kwa kuwa nimehusishwa kwenye ninahusika  jambo ambalo halihusiani nami unahitaji kukomeshwa. Ikiwa unajali sana, nimemtambulisha Michelle, usiwaze, muulize mtu wako kama alikuwa anaongea kunihusu. Kisha ondoka kwenye ukurasa wangu" Chiki alimjibu shabiki huyo.

Vile vile Michelle Ntalami alizungumzia madai hayo huku akieleza kuwa hakuwa anamzungumzia Chiki kwenye barua yake.

"Asante kwa kunitagi kwenye hii @chikikuruka! Nataka kuweka wazi jina la Chiki kutoka kwa watu wawili niliowataja kwenye barua yangu ya wazi. Yeye si mmoja wao. Zaidi ya hayo, maumivu yaliyosababishwa hayahusiani sana na wawili hao wawili ni akina nani, ni zaidi kuhusu 'wao' na mimi. Hatimaye, uamuzi wa kuwa mwaminifu daima utatokana na watu wawili walio kwenye uhusiano. Haya endelea kuangaza nuru yako @chikikuruka! Kama mshirika mwenzangu, naona na napenda unachofanyia kampuni na jamii! Nitakuwepo siku zote katika ukweli na roho." Michelle alisema.