Tafadhali njoo nyumbani,'Eric Omondi amuomba Monica Ayen arudi nyumbani wakawaone wazazi

Muhtasari
  • Eric Omondi amuomba Monica Ayen arudi nyumbani wakawaone wazazi
Eric Omondi na Monica Ayen
Eric Omondi na Monica Ayen
Image: INSTAGRAM

Kufuatia drama za hivi majuzi zinazomhusu mchekeshaji Eric Omondi, Ayen Monica, mshindi wa Wife Material 3, aliachana na Eric Omondi kupitia chapisho la Instagram.

Ayen alifichua katika chapisho siku ya Jumapili kwamba havumilii waongo, na baada ya drama zote, ilikuwa wazi kuwa Eric alikuwa mmoja.

Ayen alikuwa akizungumzia drama ya ujauzito bandia wa Eric, ambapo aliweka picha ya Miss P, mwanamuziki, akitangaza kuwa wanatarajia mtoto naye.

Walakini, baadaye ilifichuliwa kuwa hii ilikuwa tu utangazaji wa wimbo wa 'Babyshower' wa msanii huyo.

Dakika chache zilizopita, Erick Omondi amechapisha kwenye ukurasa wake rasmi wa Instagram kumtakia mpenzi wa maisha malkia wake Ayen siku njema ya kuzaliwa akionyesha mapenzi yake yote kwake.

Alimwambia arudi Kenya ili wasuluhishe masuala yao na kutoelewana kati yao ili ampeleke kwa wazazi wake waanzishe familia.

"SIKU NJEMA YA KUZALIWA MPENDWA WANGUπŸŽ‚πŸŽ‚πŸŽ‚πŸŽ‚πŸŽ‚β€β€β€β€β€. Tafadhali rudi nyumbaniπŸ‡°πŸ‡ͺπŸ‡°πŸ‡ͺπŸ‡°πŸ‡ͺπŸ‡°πŸ‡ͺπŸ™πŸ™πŸ™. Wacha tuzungumze, Tutatue Masuala yetu, tukutane na Wazazi wetu na Tuanzishe familia," Eric aliandika.

Ujumbe wake ullizua hisia tofauti na hizi hapa baadhi ya hisia zao;

mtunecessary: Lakini si ulisema wasanii wakioa tunapoteza focus? Wacha yeye kwanza tumalize shughuli lets FIX IT kwanza kiongos

finest_abuu: πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚si alikukataa

bronje.ke_: Wewe hauwezi oaπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

_star_joy: Happy birthday to her❀️

kajijoh: πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚Umekumbuka leo uliachwaπŸ˜‚πŸ˜‚

chebet_songok: Na unasema na confidence ya 82 πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚