Korti yaamuru Miss P kutoa video ya madai ya unyanyasaji wa kingono ya Willy Paul kwenye YouTube

Muhtasari
  • Korti yaamuru Miss P kutoa video ya madai ya unyanyasaji wa kingono ya Willy Paul kwenye YouTube
Willy Paul na Miss P
Image: Hisani

Mahakama ya Nairobi imeamuru Miss P aondoe video ambayo alitoa madai kuhusu Willy Paul kumnyanyasa kingono kutoka kwa mtandao wa youtube.

Miss P alitumia kurasa za vyombo vya habari na kudai kuwa mwimbaji na mtunzi maarufu wa nyimbo Willy Paul alimlazimisha kufanya naye mapenzi si mara moja na wala si mara mbili.

Alisema kwamba ilimbidi amwambie mama yake kwa sababu alipaswa kupata matibabu au vinginevyo angekuwa mjamzito.

Hii ilitokea mara baada ya Miss P kutia saini katika lebo ya Saldido records ambayo inamilikiwa na Willy Paul.

Baada ya Willy Paul kupakia uamuzi wa korti kwenye mitandao yake aliandika na kusema

"Sina mengi,wacha Mungu atende tukisonga."

Walakini Miss P alikatishwa tamaa na alichapisha meme nyingi za kusikitisha kwenye hadithi zake za Instagram akielezea jinsi alivyokuwa na huzuni lakini kila kitu kitakuwa sawa.

"Kwamba inasubiri kusikilizwa na kuamuliwa kwa shauri hili amri ya zuio inakubaliwa na kulazimisha Mshtakiwa wa Pili/Washtakiwa kufuta video iliyotumwa kwenye chaneli yake ya YouTube," ilisoma taarifa hiyo kwa sehemu.