'Nimempata mpenzi wa maisha yangu,'Harmonize afunguka kuhusu uhusiano wake mpya

Muhtasari
  • Harmonize afunguka kuhusu uhusiano wake mpya
Image: INSTAGRAM// HARMONIZE

Huku Rayvanny akiendelea kkuvuma na kugonga vichwa vya habari mitandaoni kwa madai kwamba amerudiana na mama wa mtoto wake, Fahyma. Harmonize pia ameamua kuweka wazi juu ya kupata mPenzi wa maisha yake.

Hii ni kulingana na machapisho ambayo ameshiriki kwenye mitandao yake ya kijamii ya instagram akisema kwamba amepata mwanamke wa maisha yake.

Harmonize alikuwa amechapisha picha yake na mwanamke mweupe kando yake, ambaye anadhaniwa kuwa Mpenzi wa maisha yake kama alivyosema.

Amekuwa Marekani kwa muda sasa baada ya kuondoka Tanzania kwa ajili ya kufanya ziara ya muziki, na huenda akawa anapata wakati mzuri tu kwa sasa na mpenzi wake.

Haya yanajiri baada ya kutengana na aliyekuwa mpenzi wake Kajala. Ambaye ni muigizaji wa Kitanzania na pia anatokea kuwa Mama Mpenzi wa Rayvanny.

"Hatimaye nina mwanamke wa maisha yangu," Aliandika Harmonize.

Je ni kiki msanii huyo anatafuta au ni kweli amempata mpenzi wa maisha yake?

Haya yanajiri siku moja baada yake kusema kwamba, anajuta yote ambayo yalitokea kati yake na Kajala kuhusiana na bintiye huku akimsifia kama mama bora.

"Haijalishi nini, sikufaa kureacti vile. Nahisi vibaya sana. Naona niliingiza mtu kwenye matatizo, mambo ya kupelekana kwa polisi. Nimefanya aonekane sio mama bora. Ninachoamini na najua, Kajala alikuwa anajaribu sana kwa binti yake. Alijaribu sana kumfanya bintiye bora. Naamini yeye ni mzuri" Harmonize alisema.