Samidoh na Karen Nyamu washerehekea siku ya kuzaliwa ya mtoto wao, Sam Junior

Muhtasari

•Mwanamuziki huyo wa Mugithi alitaja mwanawe kama zawadi nzuri kutoka mbinguni huku akimshukuru Mola kwa baraka hiyo

•Kwa upande wake Karen alimlimbikizia sifa mwanawe huku akiahidi kumpigania na kumpatia malezi bora.

Samidoh na Karen Nyamu
Samidoh na Karen Nyamu
Image: INSTAGRAM

Siku ya Jumapili mtoto wa mwanamuziki Samuel Muchoki almaarufu kama Samidoh na mwanasiasa Karen Nyamu aliadhimisha mwaka mmoja tangu azaliwe.

Samidoh na Karen walitumia kurasa zao za mitandao ya kijamii kusherehekea siku ya kuzaliwa ya Sam Junior kwa jumbe maalum.

Mwanamuziki huyo wa Mugithi alitaja mwanawe kama zawadi nzuri kutoka mbinguni huku akimshukuru Mola kwa baraka hiyo.

"Kila zawadi iliyo njema na kamilifu hutoka juu ikishuka kutoka kwa Baba wa mianga ya mbinguni. Ninamshukuru Mola kwa baraka zake, neema na baraka. Zawadi ya uzao, ninashukuru kwa kuongeza mshale kwenye podo langu" Samidoh aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Msanii huyo anayeshabikiwa sana haswa katika eneo la kati pia alipakia video ya mwanawe na kuiambatanisha na wimbo 'Love without End, Amen' wa George Strait ambao unazungumzia mapenzi ya baba kwa mtoto.

Kwa upande wake Karen alimlimbikizia sifa mwanawe huku akiahidi kumpigania na kumpatia malezi bora.

Karen alimtaja mwanawe kama zawadi ya thamani huku akisema alisema alimfunza upendo ambao hakuufahamu hapo awali.

"Mtoto wangu wewe ni baraka nzuri kwangu. Unastahili maisha bora zaidi. Umenifundisha upendo ambao sikujua hapo awali. Uhusiano wetu ni mojawapo ya zawadi za thamani zaidi maishani. Dadi, unaweza kunitegemea kuwa siku zote. Nitapigana vita vyako, na ikiwa nitaacha yoyote nyuma unaweza kuwa na uhakika kwamba mama alijaribu bora yake. Natarajia nyakati nzuri mbele yetu. Nakupenda sana baby. Heri ya kuzaliwa mwana! Mwanangu" Karen aliandika.

Karen na Samidoh waligonga vichwa vya habari mapema mwaka huu wakati mgombeaji huyo wa kiti cha mwakilishi wa wanawake Nairobi mwaka wa 2017 alimtaka Samidoh atambulishe mwanawe hadharani na achukue majukumu ya baba. 

Baada ya vuta nikuvute ya muda hatimaye mwanamuziki huyo alikiri kuwa baba wa mtoto huyo na kuomba familia yake pamoja na mashabiki msamaha kufuatia kitendo chake cha kuenda nje ya ndoa.

Kumekuwa na tetesi kuwa huenda wawili hao bado wako kwenye mahusiano ila bado hawajajitokeza kukubali ama kupuuzilia mbali uvumi huo.