Mastaa wa Pop, Shawn Mendes na Camilla Cabello wasitisha mahusiano yao

Muhtasari

•Mendes na Camilla wameapa kuendelea na urafiki wao licha ya kutamatika kwa mahusiano yao.

Camilla Cabello na Shawn Mendes
Camilla Cabello na Shawn Mendes
Image: GETTY IMAGES

Wanamuziki mashuhuri wa nyimbo aina ya 'Pop' Shawn Mendes na Camila Cabello wametangaza kutengana kwao baada ya kuwa kwenye mahusiano kwa kipindi cha takriban miaka miwili.

Wasanii hao wawili kutoka bara Marekani wametumia kurasa zao za mitandao ya kijamii kutangaza uamuzi wao wa pamoja wa kusitisha uhusiano wa kimapenzi.

Hata hivyo, Mendes na Camilla wameapa kuendelea na urafiki wao licha ya kutamatika kwa mahusiano yao.

"Tumeamua kusitisha mahusiano yetu ya kimapenzi lakini mapenzi yetu kwa  kila mwingine kama wanadamu yana nguvu kuliko awali. Tulianza mahusiano yetu kama marafiki wa dhati na tutaendelea kuwa marafiki wa dhati" Wapenzi hao wawili walitangaza.

Wasanii hao wamewashukuru mashabiki wao kwa kuwaonyesha upendo mkubwa na  kuwaomba waendelee vivyo hivyo.