Nitakuzaliwa watoto 2,'Akothee amwambia mpenzi wake huku akiwazomea wanaume

Muhtasari
  • Akothee amwambia mpenzi wake atamzalia watoto 2
Akothee na Nelly Oaks
Akothee na Nelly Oaks
Image: INSTAGRAM

Msanii Esther Akoth almaarufu Akothee, amelkuwa mgonjwa kwa muda sasa, huku mpenzi wake Nelly Oaks akisimama naye katika kipindi hicho kigumu.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amemshukuru sana kwa kuwa naye, huku akimhakikishia kwamba atamzalia watoto 2.

"Nakusherehekea mfalme wangu @nellyoaks hakuna mwanaume anayeweza kunistahimili kwani wengi wao wanamfuata AKOTHEE & sio Esther Akoth Kokeyo , haufuati chochote ila ustawi wangu

Ninakutangaza wewe shujaa wangu, mpenzi wangu, mpenzi wangu, mlinzi wangu na Malaika mlezi wangu! NELSON OYUGI, watoto wawili kwa ajili yako kutoka tumboni mwangu,na hakuna mtu anayeweza kuniambia masihara isipokuwa wanaweza kulipa bili zangu hata kwa siku moja tu

Asante sana kwa kunikusanya kutoka kwa takataka. Hakuna asiyefaa kama mwanamke tajiri aliyekata tamaa 🤔 Halafu ? Pesa yako haiwezi hata kusafisha uchafu wako 🤔 Mali zako haziwezi hata kukufuata kwenye kaburi lako 🤔."

 Aidaha aliwashauri 'sungle mothers' waweze kuzingatia maisha yao kwani yeye amepata yake na mpenzi wake.

"Kwa hiyo ! akina single mothers tafuteni maisha yenu kwani nishaa pata yangu @nellyoaks Mwanaume yeyote Baada yangu, Niache Peke yangu nishaachukuliwa, nipe muda na nafasi ya kupendezesha, kuzingatia na kutunza uhusiano wangu! Huwezi kutoa kile @nellyoaks anacho madukani .Nyinyi nyote nendeni kuzimu. WAHARIBIFU WA NYUMBANI," Aliandika Akothee.