Donda sugu la kuavya mimba!Nimeavya mimba mara sita sasa natamani mtoto-Mwanamke asimulia

Muhtasari
  • Mimba za mapema sio jambo geni afrika hakuna tatizo kubwa sana la wasichana wa shule kuanza uzazi wakiwa na umri mdogo 
sad woman
sad woman

Jacinta* ana umri wa miaka  30 lakini hadi  kufikia sasa ameavya mimba mara sita .

Ni ufichuzi ambao hata yeye unamshangaza kwa sababu wakati wanapofanya kitendo hicho ,haja huwa kuondoa mimba haraka anavyoweza   kwa sababu anasema hayuko tayari kumlea mtoto wala hajaolewa na hivyo basi hana uwezo wa kuanza kuwa mzazi .

Je,ilinzaje mpaka ikawa mtindo kwake kuanza kuavya mimba?

Yote yalianza akiwa shule ya msingi darasa la  nane akijitayarisha kufanya mtihani wa KCPE .kwa sababu ya shinikizo nyumbani kwamba ingekuwa aibu kwake kupata mimba akiwa shuleni na ukali wa babake ,mamake ndiye aliyempa ushauri wa kuitoa mimba hiyo na hapo ndipo alipomuua mtoto wake wa kwanza .

Akifirikia kuhusu hilo na mimba zote alizotoa hadi sasa ,anasema  endapo angewazaa wote  basi angekuwa mama wa watoto sita! Ila hali sio hiyo kwa sababu yeye nini ama marehemu kama anavyosema mwenyewe .

Mimba za mapema sio jambo geni afrika hakuna tatizo kubwa sana la wasichana wa shule kuanza uzazi wakiwa na umri mdogo .

Matarajio ya wazazi na hofu za kifamilia zikizidishwa na kuharamishwa kwa uavyaji mimba ni jambo ambalo limesababisha kuongezeka sana kwa visa vya wasichana kuavya mimba .

Anasema mimba zote alizotoa zilitokana na woga wa jinsi wazazi wake na hasa babake angelichukulia suala la yeye kwa mja mzito .

Katika visa vyote alivyopata mimba ,wanaume waliokuwa wamempachika mzigo huo nao pia hawakuwa tayari kulea watoto hao na walikuwa wepesi sana wa kutoa pesa za kwenda kufanya taratibu za kuiavya mimba .

Kutumia madaktari wanaondesha oparesheni za kuavya mimba , hilo limekuwa jambo rahisi sana kwa sababu unapogundua tu una mimba kunao madaktari wanaokupa tembe za kuitoa na pia kufanya taratibu za kusafisha uzazi wako .

Jacinta anasema aliweza kujulishwa kwa daktari wa kliniki moja mtaani aliyekuwa akiwasaidia wasichana kutoa mimba na hapo ndipo uhusiano wao ulipoanza na kila alipompigia simu kwamba na uja uzito na alitaka kuutoa ,daktari huyo alikuwa tayari kumpa usaidizi aliohitaji

Yote tisa kumi ni kuwa mwanadada huyo anasema kwamba amekuwa kwa ndoa kwa miaka 5 sasa na wala hajafanikiwa kubarikiwa na watoto, licha yake kubarikiwa na mume ambaye ana subira.