Tuheshimiane!Hamisa Mobetto awaonya wanaomhusisha na wanaume asiowajua

Muhtasari
  • Anasema kwamba wale wanaomhusisha na wanaume ambao hawachumbii wakome
  • Kwa maana hafurahishwi na watu hao wanaounganisha picha yake na wanaume ambao hawachumbii nao
Hamisa Mobetto
Image: INSTAGRAM

Hamisa Mobetto hana furaha  hii baada ya kupitia kwenye mtandao wake wa kijamii kuwakashifu watu wanaomhusisha na hadithi ambazo hajui chochote kuzihusu.

Anasema kwamba wale wanaomhusisha na wanaume ambao hawachumbii wakome.

Kwa maana hafurahishwi na watu hao wanaounganisha picha yake na wanaume ambao hawachumbii nao.

"Ifike mahali uache kuunganisha picha zangu na wanaume ambao sina ukaribu naowala kufahamiana nao vizuri

Tuheshimiane tafadhali kila siku inachosha, kukyta picha zangu zinaunganishwa ovyo,na muache kunitungia story jamani mimi mwenyewe staring nakua sijui hiyo movie nimeicheza wapi na saa ngapi," Alisema Hamisa.

Aliongeza kuwa kuna wakati alipotea kwenye mitandao ya kijamii na watu walifikia kumpa ujauzito kitu ambacho si kweli hata kidogo.

Akiongeza kuwa wale wanaompenda tu ndio wamuite 'Missa' kwa kuwa si jina la kila mtu.

Kwa watu maalum tu, na kwamba wale wanaotengeneza hadithi za uwongo juu yake wanapaswa kuacha kwani mwisho wa siku watachanganyikiwa.