"Tumieni akili, mmekosa kazi!" Zari akemea wanaomkosoa kwa kuvaa chupi nyeusi ndani ya nguo nyeupe

Muhtasari

•Kwenye video hiyo ambayo ilirekodiwa wakati wa sherehe za kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa, Zari anaonekana akiwa anasakata densi huku akiwa amevalia nguo nyeupe pe!

•Baadhi ya wanamitandao na wanablogu  wamekuwa wakikosoa chaguo la Zari kuvalia nguo nyeupe ilhali ndani yake kavalia chupi nyeus

Image: INSTAGRAM// ZARI HASSAN

Mwanasoshalaiti na mjasiriamali Zari Hassan amewakemea watu ambao wamekuwa wakimkosoa baada ya video inayoonyesha chupi aliyovalia kusambaa mitandoni.

Kwenye video hiyo ambayo ilirekodiwa wakati wa sherehe za kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa, Zari anaonekana akiwa anasakata densi huku akiwa amevaa nguo nyeupe pe!

Katika harakati ile ya kucheza densi  mpenzi huyo wa zamani wa Diamond Platnumza anagusa nguo yake ambayo inainuka juu kiasi na kuonyesha chupi nyeusi aliyokuwa amevalia. 

Baadhi ya wanamitandao na wanablogu  wamekuwa wakikosoa chaguo la Zari kuvalia nguo nyeupe ilhali ndani yake kavalia chupi nyeusi.

Zari ametumia ukurasa wake wa Instagram kuwakemea wakosoaji wake huku akitetea chaguo ya mavazi yake.

"Watu wanauliza eti mbona nivae chupi nyeusi. Nilikuwa nimevaa nguo nyeupena ningevaa chupi nyeupe ingeacha alama. Huwa namwambia mtumie akili. Akili ya kawaida si kawaida lakini tumieni akili. Huwezi valia chupi nyeupe ndani ya nguo nyeupe" Zari alijitetea.

Zari amesema wanaochukua wakati wao kukejeli mavazi yao wanafanya vile kwa kuwa wamekosa kazi.

"Mmekosa kazi. Hata kama ni blogu, mmekosa cha kusema. Tumia muda unaotumia kwangu kwako mwenyewe. Hata kama ni mwezi mmoja tu. Utaona mabadiliko maishani" Zari amesema.