"Huyo hatawahi nona, udaku umekula nyama zote!" Willy Paul amshambulia Eric Omondi

Muhtasari

•Kulingana na Willy Paul, udaku mwingi wa Omondi umefanya mwili wake ukasita kunenepa na atasalia kuwa mkonda iwapo hataacha udaku.

•Willy Paul alisema wasanii wengi walisita kuunga mkono kampeni ambayo Eric anaendeleza kwa kuwa mchekeshaji huyo alikusa mpangilio mzuri alipokuwa ananza.

Willy Paul, Eric Omondi
Willy Paul, Eric Omondi
Image: INSTAGRAM

Mwanamuziki wa nyimbo za kisasa Wilson Radido almaarufu kama Willy Paul amezungumza kuhusu drama za hivi majuzi mitandaoni kati yake na mchekeshaji Eric Omondi.

Alipokuwa anahutubia wanahabari baada ya hafla ya kuzindua albamu yake mpya 'The African Experience' siku ya Jumamosi, Willy Paul alimtaja Eric kama mtu mwenye udaku mwingi sana.

Kulingana na Willy Paul, udaku mwingi wa Omondi umefanya mwili wake ukasita kunenepa na atasalia kuwa mkonda iwapo hataacha udaku.

"Achana na Eric. Mnadhani mbona hanoni? Huyo hatawahi nona, udaku umekula nyama yote kwa mwili. Si rahisi kujua ako na miaka 52, sitarajii mtu wa miaka 52 awe anaongea hivo!" Willy Paul alisema.

Mwanamuziki huyo amemsihi Eric Omondi abadili tabia zake kwani haziambatani na umri wake.

'"Eric unahitaji kuwa mwanaume! Man up! Babu! ako 52!" Alisema Willy Paul.

Hata hivyo, Paul ameunga mkono muswada ambao Eric alikabidhi wabunge Babu Owino na Charles Njagua wiki iliyopita unaopendekeza vituo na maeneo ya burudani nchini yacheze asilimia 75 ya muziki ulioimbwa na wasanii wa Kenya kila wakati.

Willy Paul amesema hatua ambayo Eric alipiga ni nzuri huku akisema wanamuziki wa Kenya wataweza kushabikiwa zaidi nyumbani iwapo muswada huo utapitishwa bungeni.

"Anachofanya ni kitu poa. Ikipita itakuwa sawa sana, hivo ata mashabiki wetu watazoea. Unajua mashabiki wetu ukiwauliza kama wanataka ngoma za hapa ama za kitaifa watasema za kitaifa. Sababu ni kuwa wamefanywa wasikie muziki wa kimataifa sana kuliko wa hapa nchini hata wanadharau wasanii wao" Alisema Willy Paul.

Willy Paul alisema wasanii wengi walisita kuunga mkono kampeni ambayo Eric anaendeleza kwa kuwa mchekeshaji huyo alikusa mpangilio mzuri alipokuwa ananza.

"Aliiweka vibaya. Aliiweka ikakaa ni kama ni yeye anaifanya. Ndio maana hata wasee wengine walikuwa wanaogopa"