"Yeye pia ni damu yangu!" Milly Wajesus afunguka kuhusu uhusiano wake na binti ya mumewe, Abby

Muhtasari

•Mama huyo wa mtoto mmoja alisema anamchukulia Abby kama binti yake tu kwa sababu ndoa ilimuunganisha pamoja na Kabi.

•Kabi naye alisema jambo la ushirikiano kwenye malezi ni geni kwake  huku akifichua huwa anavutiwa sana na jinsi Bahati hushirikiana vizuri na baby mama wake Yvette Obura kulea binti yao Mueni Bahati.

Kabi Wajesus, Milly Wajesus
Kabi Wajesus, Milly Wajesus
Image: INSTAGRAM

Mwanavlogu Millicent Wambui almaarufu kama Milly Wajesus amefunguka kuhusu uhusiano wake na binti ya mumewe Kabi Wajesus, Abby.

Akiwa kwenye mahojiano na SPM Buzz, Milly aliweka wazi kwamba tayari amemkubali Abby kuwa sehemu ya familia yake.

Mama huyo wa mtoto mmoja alisema anamchukulia Abby kama binti yake tu kwa sababu ndoa ilimuunganisha pamoja na Kabi.

"Abby ni kama binti yangu. Maadamu yeye ni damu ya mume wangu, yeye ni damu yangu pia. Hii ni kwa sababu tulipokuja pamoja tulifanywa kitu kimoja. Naamini hivo" Milly alisema.

Milly alisema haikuwa ngumu sana kumkubali Abby katika familia yake kwa kuwa amekua pamoja na watu wasio wa damu yake.

"Watu hawajui kunihusu. Ambako nimetoka nimeishi na watu ambao hawakuzaliwa na wazazi wangu. Nimeishi na watu watatu kufikia sasa. Nimezoea kukubali watu ambao napenda. Nimezoea kuwa na familia kubwa. Kwangu Abby ni sehemu ya familia yangu" Alisema Milly.

Kabi naye alisema jambo la ushirikiano kwenye malezi ni geni kwake  huku akifichua huwa anavutiwa sana na jinsi Bahati hushirikiana vizuri na baby mama wake Yvette Obura kulea binti yao Mueni Bahati.

"Ningependa kukaa chini na Bahati nijue namna ya kuwa mzazi mwenza. Hilo ni jambo geni kwake sasa. Huwa naona anaweza kufanya mambo mengi na mtoto wake. Ningependa kujifunza mambo kadhaa kutoka kwao" Alisema.

Wiki iliyopita wanandoa hao walimkaribisha Abby katika familia yao ya mitandaoni, The Wajesus family.