Mike Sonko aomba kusaidiwa kupatana na mganga anayedaiwa kutumia nyuki kukamata wezi ili ampatie kazi

Muhtasari

• Alipakia video ya kutisha  ya mganga  kutoka Mwingi  ambaye anaonekana akimeza nyoka aliye hai na kuiambatanisha na ombi la kusaidiwa kupata naye ili ampatie kazi ya kunasa mwizi.

•Sonko alisema rafiki yake angetoa zawadi ya shilingi 250, 000 kwa amtu yeyote ambaye angetoa habari za kuaminika ambazo zingesaidia kupatikana kwa mali iliyoibiwa.

Mike Sonko na Screenshoot ya video ya mzee anayemeza nyoka ambayo aliyopakia
Mike Sonko na Screenshoot ya video ya mzee anayemeza nyoka ambayo aliyopakia
Image: FACEBOOK// MIKE SONKO

Aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko ametoa wito kwa Wakenya kumsaidia kupatana kukutana na mganga anayedaiwa kutumia nyuki kuwashika wezi.

Kwenye mtandao wake wa Facebook Sonko alipakia video ya mzee mmoja anayeaminika kutoka eneo la Mwingi  ambaye anaonekana akimeza nyoka aliye hai na kuiambatanisha na ombi la kusaidiwa kupata naye ili ampatie kazi ya kunasa mwizi.

"Naskia huyu mzee ni yule anashikanga waizi na nyuki. Hebu aletwe haraka upesi nimpe kazi. Ni watu wangapi hii kanairo mumeibiwa?" Sonko aliandika chini ya video hiyo.

Hapo awali mwanasiasa na mfanyibiashara huyo alikuwa ametangaza kwamba rafiki yake kutoka Ujerumani aliibiwa seti 25 za samani katika eneo lake la biashara mtaa wa Shanzu, Mombasa.

Naskia huyu mzee ni yule anashikanga waizi na nyuki. Hebu aletwe haraka upesi nimpe kazi. Niwatu wangapi hii kanairo mumeibiwa?

Posted by Mike Sonko. on Friday, December 3, 2021

Sonko alisema rafiki yake angetoa zawadi ya shilingi 250, 000 kwa amtu yeyote ambaye angetoa habari za kuaminika ambazo zingesaidia kupatikana kwa mali iliyoibiwa.

"Inatuhumiwa ziliuziwa mmiliki mmoja wa klabu/hoteli eneo la Pwani Kaskazini. Tupigie simu 0724354400/ 0736935711/ 0711120001" Alisema Sonko.

Aliambatanisha tangazo hilo na picha za samani zinazodaiwa kuibiwa katika eneo la biashara la rafiki yake.