"Umenionyesha kupendwa ni nini kwa njia nyingi tofauti!" Diana Marua amlimbikizia mpenziwe Bahati sifa kochokocho

Muhtasari

•Rapa huyo chipukizi ametumia ukurasa wake wa Instagram kumshukuru baba ya watoto wake wawili kwa kuwa msukumo mkubwa katika maisha yake na kumbwagia mapenzi yasiyo na kipimo.

•Amesema mumewe sio mtu wa kawaida tu wala wa kufananishwa na yeyote huku akiapa kuendelea kusimama naye kila wakati na kuwa mke mtiifu.

Image: INSTAGRAM// DIANA MARUA

Licha ya hisia tofauti ambazo zimechimbuka mitandaoni haswa  baada ya Diana Marua kujitosa kwake kwenye muziki, mpenzi wake Bahati bado ameendelea kumshikilia mkono na kuhakikisha mkewe amepata kufanikiwa.

Diana Marua ambaye kwa sasa anajitambulisha kwa jina la jukwaani Diana B ameridhishwa sana na mapenzi makubwa ambayo mume wake ameendelea kumuonyesha na jinsi amekuwa akimsukuma awe bora

Rapa huyo chipukizi ametumia ukurasa wake wa Instagram kumshukuru baba ya watoto wake wawili kwa kuwa msukumo mkubwa katika maisha yake na kumbwagia mapenzi yasiyo na kipimo.

"Mume Wangu, Rafiki Yangu Kipenzi, Mshauri Wangu, Nguzo Yangu, Baba Wa Watoto Wangu, Padri Wa Nyumbani Kwetu. Nakupenda❤️ Ninavutiwa na jinsi unavyonionyesha kwa Ulimwengu, jinsi unavyonipenda, jinsi unavyonisukuma kuwa bora zaidi, jinsi unavyozungumza nami usiku mwingi ili kunisifu, jinsi unavyoniambia unavyonipenda kwa matendo yako na zaidi kuhusu jinsi unavyotamani kuniona nikisimama juu ya neno MAFANIKIO na Taa za Kijani juu yangu" Diana alimwandikia Bahati.

Diana amesema mumewe sio mtu wa kawaida tu wala wa kufananishwa na yeyote huku akiapa kuendelea kusimama naye kila wakati na kuwa mke mtiifu.

"Naahidi Kama vile ulivyoniunga mkono, nitakuunga mkono daima, nitasimama nawe daima, nitakufanya ufurahie. Umeweka kila kitu pembeni kuhakikisha nashinda katika Maisha yetu. Wewe ni wa ajabu, haufananishwi na yeyote, hakuna anayekufikia!Umenionyesha kupendwa ni nini kwa njia nyingi tofauti. Katika safari hii ambayo Mungu ametufanyia, nitakuwa mtiifu kwako kila wakati kama vile Biblia inavyoniamuru. KWA YOTE NATAKA KUSEMA ASANTE. NIKO KWA AJILI YA KUKUFANYA. IFURAHI, NAKUPENDA @BAHATIKENYA" Amesema Diana.

Bahati amemjibu mpenzi wake kwa kumhakikishia kwamba anampenda na anajivunia sana kuitwa mume wake.