" Hatuko pamoja tena!" Carrol Sonnie athibitisha kutengana na Mulamwah miezi baada ya kukaribisha kifungua mimba

Muhtasari

•Ingawa hajafichua sababu za kutengana kwao, Muthoni amesema walifanya makubaliano ya pamoja huku akimshukuru baba ya binti wake kwa kipindi cha miaka minne ambacho wamekuwa pamoja.

•Mwaka uliopita walikuwa wametengana tena kwa kipindi kisha wakarudiana ila hawakufichua kilichokuwa kimewatengisha.

Image: INSTAGRAM// MULAMWAH

Takriban miezi miwili tu baada ya kukaribisha mtoto wao wa kwanza, ni dhahiri kwamba mahusiano kati ya mchekeshaji Mulamwah na mpenzi wake Caroline Muthoni yamefika hatima.

Bi Muthoni ambaye anafahamika zaidi kama Carol Sonnie ametumia ukurasa wake wa Instagram kuthibitisha kutengana kwao.

Ingawa hajafichua sababu za kutengana kwao, Muthoni amesema walifanya makubaliano ya pamoja huku akimshukuru baba ya binti wake kwa kipindi cha miaka minne ambacho wamekuwa pamoja.

"Hii ni kuweka wazi kuwa mimi na Mulamwah hatuko pamoja tena. Sote tumekubaliana na kuamua kuachana kwa sababu zinazojulikana kwetu. Asante sana kwa upendo na usaidizi mliotupa kwa miaka hiyo 4, mimi binafsi sichukulii kawaida.

Kwa mulamwah, Asante sana kwa kuniruhusu kuwa sehemu ya maisha yako kwa miaka hiyo.  Nashukuru sana na nitahifadhi kumbukumbu milele. Katika hatua yako inayofuata maishani, sikutakii kingine ila bora.Endelea kushinda na Mungu akubarikikatika  kila hatua ya maisha yako" Muthoni ameandika.

Muthoni amesema ataendelea na kazi zake kivyake huku akisihi mashabiki kuendelea kumuonyesha upendo kama awali.

"Kwa mashabiki wangu, asante kwa sapoti yenu na upendo ambao mmekuwa mkinionyesha. Mungu awabariki kila mmoja wenu. Nikiendelea na safari hii niruhusu niwe nashika simu zenu zenye vitu vya ajabu na najua kwa hakika mtapenda😊. Kuvunjika kwa mwiko sio mwisho wa kupika ugali so we MOVE FORWARD and pray for better tomorrow😍 . Endelea kuunga mkono na kuonyesha upendo. Kazi izidii!" Amesema Carrol.

Wapenzi hao walikaribisha mtoto wao wa kwanza wa kike, Keilah Oyando mnamo Septemba 20 mwaka huu.

Mwaka uliopita walikuwa wametengana tena kwa kipindi kisha wakarudiana ila hawakufichua kilichokuwa kimewatengisha.