Tuache 'beef' za kijinga,'beef' yangu na wewe imeisha-Willy Paul amwambia Eric Omondi

Muhtasari
  • Willy Paul amshauri Eric Omondi wamalize ugomvi wao
Image: INSTAGRAM// WILLY PAUL, ERIC OMONDI

Willy Paul amewaacha wanamitandao  wakizungumza kwenye mitandao ya kijamii kwa mara nyingine. Hii ni baada ya kumwambia Eric Omondi kukatisha rasmi ugomvi wao.

Kulingana na maoni ambayo Willy alitoa kwenye chapisho la Eric Omondi, msanii huyo  alikuwa akimshukuru Eric Omondi kwa kushiriki wimbo wake kwenye akaunti yake, jambo ambalo lilimfanya Willy Paul kushukuru.

"Hizi ndio vitu tunataka Kwa Industry. Watu wajitume kabisa. Naona Ulishoot Video Russia...Endelea hivyo hivyo. Mimi kitu tu nataka ni tuvuke ma Border na tuheshimiwe INTERNATIONALLY.🇰🇪🇰🇪🇰🇪🇰🇪," Aliandika Eric.

Sasa kauli hii ya Willy Paul kuhusu mwisho wa tofauti zake na Eric imeenea kwenye mitandao tofauti ya kijamii ambapo, inazua hisia tofauti kwa sasa.

"Asante ndugu yangu, tuache beef za ujinga na tuinue tasnia yetu vile umesema.. tufike International standards. asante kwa kuniunga mkono mimi beef yangu na wewe imeisha officially.. endelea kufanya kile unafanyamanze. Endelea kuunga mkono tasnia ya muziki... sinapata support kwa album yangu ya #THEAFRICANEXPERIENCEALBUM na hizi ndio song ziko ndani.. yaani wewe, @mainawakageni na @arrowbwoy ndio wasee tu wametaja... na msichana wetu @mungai_eve .. I'm humbled and sitawai kata tamaa ata iwe nini.. one man army," Alijibu Willy Paul.