“Hatuachani ng’o!” Bahati awajibu mahasidi wanaotaka ndoa yake na Diana Marua isambaratike

Muhtasari

•Alisema wanaotaka waachane ni watu wasio na uwezo wa kifedha na wasioweza kugharamia mahitaji ya mke wake.

Image: INSTAGRAM//DIANA MARUA

Baada ya kimya kirefu msanii Bahati amejitokeza wazi na kuzungumzia drama ambazo zimekuwa zikienea mitandaoni zinazomhusisha pamoja na mkewe Diana Marua na Willy Paul.

Kupitia video iliyopakia kwenye mitandao ya kijamii, Bahati alisema madui wake wamekuwa wakitaka wachane na Diana jambo ambalo amesema aliwenzekani kabisa.

“Nataka kusema siombi msamaha kwa yeyote hapo nje. Mnataka niombe msamaha na hatujakosana na bibi yangu? Kwani nyinyi ni wazimu. “ Bahati alisema.

Alisema wanaotaka waachane ni watu wasio na uwezo wa kifedha na wasioweza kugharamia mahitaji ya mke wake.

"Nawauliza kama mwajua ilivyo ghali kuwa na Diana. Kama nikimpea huyu msichana mtaweza kumdumisha kweli? Mnajua alivyo ghali? Tafadhali endeleni na maisha yenu... mbona mlisema tulifanya hivo hili tujulikane si pia nyinyi muachane na wake zenu tuone kama mtajulikana” Alisema.

Hivi karibuni Diana Marua amekuwa akivuma mitandaoni haswa baada ya kutoa madai kuwa Willy Paul aliwahi kujaribu kumbaka.

Wanamitandao hawajasalia nyuma katika kutoa hisia mbalimbali kuhusu jambo hilo wengine wakikejeli huku wengine wakionekana kuegemea upande fulani.

Licha ya yote Bahati amesisitiza kwamba haachani na mkewe liwe liwalo