'Kusafiri hutuongezea ladha kwa tendo la ndoa,' Kabi na Milly Wajesus watoboa siri zao za kitandani

Muhtasari

•Walisema wakati walipokuwa wanajiandaa kufunga pingu za maisha walitazamia kuwa wanashiriki tendo hilo angalau mara tatu kwa siku ila wakakiri kwa sasa hali sio kama walivyofikiria ingekuwa.

•Kabi na Milly waliweka wazi kwamba huwa wanafurahia tendo la ndoa zaidi kila wanaposafiri kwani huwa madhari mapya yana mazoea ya kuwasisimua zaidi.

Image: INSTAGRAM// MILLY WA JESUS

Wanandoa mashuhuri Peter Kabi na Millicent Wambui wa 'The Wajesus Family' wamefunguka kuhusu ndoa yao ya miaka minne.

Hivi majuzi wawili hao walitumia YouTube channel yao kujibu maswali mbalimbali ambayo mashabiki wao wamekuwa wakitaka kufahamu kuhusu ndoa yao.

Shabiki mmoja alitaka majibu kuhusu hali ya tendo la ndoa kati ya wanandoa hao  na njia ambazo huwa wanatumia kuliongeza ladha zaidi.

Wazazi hao wa mvulana mmoja, Reign Taji  hawakusita kufichua siri kadhaa za kitandani huku wakiweka wazi kwamba wanaendelea kufurahia tendo hilo haswa kila wanaposafiri.

"Tuko sawa katika tendo la ndoa. Nadhani  huwa tunafurahia zaidi wakati tumesafiri ama tukiwa katika likizo.Wakati huo huwa tuko na siku nzima na muda mwingi. Mtu hufikiria akioa itakuwa twa! twa! twa!.. Ndoa iko na kazi mingi. Huenda kuna mambo mingi ambayo mnafanya pamoja ambayo itawazuia kukosa kushiriki tendo la ndoa kila siku. Haiwezi" Kabi alisema.

Walisema wakati walipokuwa wanajiandaa kufunga pingu za maisha walitazamia kuwa wanashiriki tendo hilo angalau mara tatu kwa siku ila wakakiri kwa sasa hali sio kama walivyofikiria ingekuwa.

Walisema tendo la ndoa huendelea kuridhisha zaidi kadri ndoa inavyoendelea kukua kwani wanandoa huendelea kufahamiana zaidi.

"Tumejua mengi kuhusu mwingine. Imeendelea kuwa nzuri zaidi. Kwa sasa kila mmoja wetu anajua wapi pa kugusa ili kufika wapi. Kila kitu ni kinalingana na uzoefu" Milly alisema.

Kabi na Milly waliweka wazi kwamba huwa wanafurahia tendo la ndoa zaidi kila wanaposafiri kwani huwa madhari mapya yana mazoea ya kuwasisimua zaidi.

"Kusafiri huboresha tendo letu la ndoa. Mimi napenda maeneo tofauti, napenda mabadiliko. Wakati mwingin unawezaboeka kuona kila wakati ni paa ileile, taa ileile, kitanda kilekile. Haswa ukiwa nyumbani kuna watoto na watu wengine huwezi enda mahali mbalimbali kwa nyumba. Tukisafiri huwa tunaenda sehemu mbalimbali za nyumba. Hivo ndivyo huwa tunaongeza ladha!" Milly alisema.

Wawili hao walisema ndoa yao haijakuwa paradiso kila wakati na kukiri kwamba huwa wanatofautiana mara kwa mara. Hata hivyo waliweka wazi kwamba huwa hawapigani vita vya kimwili.