"Nitachukua hatua mbaya sana!" Bilionea Grand P ampa onyo kali mwanamuziki aliyempokonya mke

Muhtasari

•Picha za mwanasoshalaiti Eudoxie Yao pamoja na Roga Roga ambazo zimekuwa zikienezwa mitandaoni zimemtia hofu kubwa Grand P kwamba  msanii huyo kutoka Kongo huenda akampokonya jiko lake.

Grand P, Eudoxie Yao na Roga Roga
Grand P, Eudoxie Yao na Roga Roga
Image: FACEBOOK

Mwanamuziki na mwigizaji mashuhuri kutoka Guinea Moussa Sandiana Kaba almaarufu kama Grand P ni mwenye ghadhabu isiyodhibitika baada ya kuona kama kwamba msanii mwenzake kutoka Kongo Roga Roga anamezea mate kipenzi chake Eudoxie Yao.

Picha za mwanasoshalaiti Eudoxie Yao pamoja na Roga Roga ambazo zimekuwa zikienezwa mitandaoni zimemtia hofu kubwa Grand P kwamba  msanii huyo kutoka Kongo huenda akampokonya jiko lake.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Bilionea huyo mwenye maumbile ya kipekee amempatia Roga Roga onyo kali  dhidi ya kuendeleza mahusiano na mkewe 

Grand P amesema ingawa ana heshima kubwa kwa Roga Roga pamoja na Wakongo wote hatasita kuchukua kali iwapo mwanamuziki huyo ataendelea kutongoza kipenzi chake.

"Ndugu yangu Roga Roga nakuheshimu sana wewe na watu wote wa Kongo... Lakini  njia unayotaka kufuata si ya kupendeza kwako, usifurahie kuwa karibu na mke wangu la sivyo nitachukua hatua mbaya. Hii ni onyo, Asante!" Grand P aliandika.

Grand P aliambatanisha ujumbe wake na picha mbili zilizoonyesha akiwa anafanya mazoezi katika Gym na ingine moja iliyoonyesha Roga Roga pamoja na Eudoxie Yao.

Grand P na Yao ambaye amebarikiwa na makalio makubwa kweli wamekuwa kwenye mahusiano kwa kipindi kirefu huku wakionekana kukosa na kurudiana mara kwa mara.