Ni mrembo!Vera Sidika amtambulisha mwanawe kwa mara ya kwanza kwa mashabiki

Muhtasari
  • Hata hivyo Vera hakuhisi uchungu wowote kwa sababu alichagua tarehe yake ya kuwasili kibinafsi
Image: INSTAGRAM// VERA SIDIKA

Mwanasosholaiti Vera Sidika na mumewe mwimbaji Brown Mauzo wametambulisha uso wa binti yao Princess Asia Brown kwa mara ya kwanza tangu kuwasili kwake.

Asia alizaliwa tarehe 10/10/2021 chini ya matukio ya kipekee.

Ilikuwa ya kipekee kwa sababu mama yake aliruhusiwa kuingia kwenye chumba cha kujifungulia na vipondozi,  na wigi.

Hata hivyo Vera hakuhisi uchungu wowote kwa sababu alichagua tarehe yake ya kuwasili kibinafsi.

Sidika anajulikana sana kwa maisha yake ya kutatanisha. Aliwahi kuibuka akidai kuwa amejipaka ngozi na mamilioni ya pesa hivyo alipopata ujauzito, wanamtandao walitabiri kuwa mtoto wake atakuwa na rangi yake ya asili.

Hata hivyo, kwa mshangao wao, binti yake ni mrembo sana. Pengine, alichukua rangi ya baba yake.

Vera na mumewe brown Mauzo wamekuwa kwenye ndoa kwa takriban miaka miwili sasa. Upendo wao kwa kila mmoja wao unaonekana kukua kila siku.

"Mungu ametupa kipande chake cha mbinguni. Kutana na Asia Brown @princess_asiabrown link kwenye bio," Aliandika Vera.

Kutana na binti yao mrembo