- Wanamitandao wasifia urembo wa mwanawe mwanasosholaiti Vera Sidika
Mwanasosholaiti Vera Sidika Jumatatu kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram alitambulisha picha ya mwanawe kwa mara ya kwanza.
Vera wakiwa na mume wake, Brown Mauzo walionyesha sura ya mwanao kwa mara ya kwanza huku Vera akionyesha furaha kubwa kwa maandishi yaliyoambaatana na picha ile ya kifungua mimba wao
Ikumbukwe wanamitandao wamekuwa wakitoa maneno mbalimbali huku wakitaka kujua mtoto Asia anafanana na nani baina ya wazazi hao wawili.
Sidika anajulikana sana kwa maisha yake ya kutatanisha. Aliwahi kuibuka madai kwamba ametumia mamilioni ya pesa kubadilisha mwonekano wake wa ngozi huku wanamtandao wakitabiri mtoto wake atakuwa na rangi ya asili .
Wanamitandao hawakubaki nyuma kutoa kauli zao ambazo zilikuwa kinyume na matarajio kwani mtoto huyo alikuwa amependeza ajabu huku wengine wakisema mtoto amechukua sura ya baba yake, Brown Mauzo
Baadhi za ujumbe ya wanamtandao ni kama;