Wanaume wote wanajua hawawezi kuwa waaminifu kwa mwanamke mmoja-Huddah Monroe adai

Muhtasari
  • Mwanasoshaolaiti Huddaha adai hamna mwanamume ambaye ni mwaminifu
  • Matamshi yake yanajiri saa chache baada ya kudai kwamba anauza tumbo la uzazi
Image: INSTAGRAM// HUDDAH MONROE

Mwanasosholaiti Huddah Monroe amewaacha mashabiki wake na hisia tofauti baada  ya kusema  kwamba hawezi kuwa kwenye ndoa.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram, kwenye sekta ya hadithi za instagram HUddah alisema kwamba wanaume wanafahamu vyema kwamba hawawezi kuwa waaminifu kwa mwanamke mmoja.

Matamshi yake yanajiri saa chache baada ya kudai kwamba anauza tumbo la uzazi.

"Zaidi ya yote wanaume wanajua kwamba hawawei kuwa waaminifu kwa mwanamke mmoja,na wanadai kwamba ni biolijia ikizungumzia kuwa hivyo ndivyo wameumbwa

Wacheni kuwashinikiza wanawake,tuambieni moja kwa moja kwamba mna wengine 3 utakuwa wa nne? tukubaliane kutokubaliana," Huddah Amesema.

Huddah aliwaambiwa wanaume kwamba hana shida na wao kuwa na wanawake kumi kwani huwa inaokoa wakati wao.

"Hatuna shida nanyi mkiwa na wanawake kumi,waekeni, huwa inaokoa muda wenu , nitaamua mapema kama nitakuwa na wewe John au James sio baada ya kupata hisia 

Napata kuwa una baby mama 5, watoto 25 na wake 6."