Hatukuachana na Mulamwah kwa ajili ya Keilah-Carol Sonie awasuta wanaoeneza habari za uongo

Muhtasari
  • Carol Sonie awasuta wanaoeneza habari za uongo
Image: INSTAGRAM// CAROL SONNIE

Carol Sonnie, mpenzi wa zamani wa Mulamwah amejibu madai kwamba alitengana na babake mtoto kutokana na maswali kuhusu baba wa binti yao.

Tetesi zilienea kuwa Mulamwah alikuwa na DNA na akagundua kuwa hakuwa baba Keilah, jambo ambalo baby mamake amekanusha vikali.

Katika video, Sonnie alitaja madai hayo kama habari za uongo na kuwataka wanaoeneza habari hiyo kuacha mara moja.

“Kuna hawa mahususi wanaosambaza taarifa za uongo za kwa nini niliachana na Mulamwah sijui wanatafuta cha kusema

Acha niweke wazi, sababu iliyonifanya kuachana na Mulamwah sio Keilah na ni mtoto wa Mulamwah

Kwa nini utoe maoni kama haya, nimekuwa nikipigiwa simu nyingi na jamaa zangu wakiuliza ikiwa habari hizo ni za kweli. Sijawahi kutoa maoni kama haya

Acha kuniharibia jina, acha kuchafua jina la Mulamah, acha kuchafua jina la Keilah. Kwa ajili ya Mungu, sio jambo la kuchekesha hata kidogo. Unajaribu kufanya nini? Acha Ujinga bwana, ukue," Alisema Sonie.