Hongera! Larry Madowo abarikiwa na mtoto wa kiume

Muhtasari

•Mtangazaji huyo wa zamani wa NTV na BBC amekuwa akiweka maisha yake ya mahusiano kama siri na kufuatia hayo mzazi mwenza wake bado hajatambulika.

Image: FACEBOOK// LARRY MADOWO

Mtangazaji maarufu wa CNN kutoka Kenya Larry Madowo ametangaza kuzaliwa kwa mtoto wake wa kwanza.

Mtangazaji huyo mwenye umri wa miaka 34 ametumia ukurasa wake wa Facebook kutangaza baraka ya mtoto wa kiume.

"Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, tumebarikiwa na mtoto mwanamume" Madowo aliandika chini ya picha yake akiwa ameshika kitoto kwenye mikono yake.

Mtangazaji huyo wa zamani wa NTV na BBC amekuwa akiweka maisha yake ya mahusiano kama siri na kufuatia hayo mzazi mwenza wake bado hajatambulika.

Wanamitandao wengi wamejumuika chini ya tangazo la Madowo wakimwandikia jumbe za pongezi huku wengine wengi wakimuomba atambulishe mpenzi wake.

Hizi baadhi ya jumbe za wanamitandao

@Hesborn Etyang Ni mshangao ulioje! Hongera

@Justice Kirui Hongera sana. Mpe jina Emannueli kwa sababu alizaliwa siku mbili baada ya kuzaliwa kwa Yesu

@Sarah Nduku Hongera sana Larry. Sasa wanawake wengine wanaweza kupumzika na kupumua

@MrRightKe Larry Madowo ana mtoto mchanga na wanawake wa Kenya hawana furaha hata kidogo

@osoriojnr Larry Madowo awatania mashabiki wake kwa picha akiwa amemshika mtoto mchanga. Ama Edith kimani alikuwa mjamzito?