Mwanamuziki sifika duniani Drake Graham almaarufu Drake, siku ya Jumapili akiwa maeneo ya Toronto nchini Canada alionekana akigawa pesa barabarani nchini humo.
Katika ukurasa wake wa Instagram rapa huyo mzaliwa wa Canada alipakia video fupi ambayo ilionyesha akitumia siku yake ya Krismasi kugawa pesa kwa wakazi.
Video mbili ambazo alipakia Instagram akigaawa pesa siku ya Krismasi zilidhirisha upendo mkubwa anao kwa mashabiki wake.
Mwanamuziki huyo ambaye nyimbo zake zinapendwa dunia nzima kwa mtindo wake wakuimba amevutia wengi kwa kitendo hicho cha hisani
Hata hivyo haijabainika kiwango cha pesa msanii huyo wa Kimataifa alitumia siku hiyo ya Boxing Day kutunuku watu waliokuwa Barabarani wakati alipokuwa akipita.