Tetesi zaibuka kuwa Nadia Mukami ni mjauzito

Muhtasari

•Mtindo wa mavazi wa mwanamuziki wa hivi majuzi umeanza kuibua tetesi kwamba huenda  mwimbaji  huyo anatarajia mtoto hivi karibuni.

Nadia Mukami
Image: INSTAGRAM

Mwanamuziki mashuhuri  Nadia Mukami  almaarufu  Nadia Katamu hivi karibuni amewacha mashabiki wake na maswali chungu nzima, haswa wanamitandao kutokana na mtindo wake mpya wa mavazi. 

Mtindo wa mavazi wa mwanamuziki wa hivi majuzi umeanza kuibua tetesi kwamba huenda  mwimbaji  huyo anatarajia mtoto hivi karibuni.

Mapema mwaka huu Nadia alipasua mbarika kuhusu mahusiano yake na msanii mwenzake wa humu nchini, Arrow Bwoy.

Video yake akitumbuiza mashabiki  mjini  Eldoret imewafanya wengi kuwa na maswali bila majibu yaliyothibitishwa huku wengine wakimpongeza  kwa  ujauzito .

kupitia mtandao wake wa Istagram mashabiki walimpongeza huku wengine wakitaka awaeleze ukweli kama ana ujauzito.

Siku alikuwa Eldoret alipanda jukwaani akiwa amevalia sweta iliyolegea na kaptura nyeusi, ambapo alipokelewa na mpenzi wake Arrow Bwoy na kuanza kuwatumbuiza mashabiki waliojitokeza kwa siku hio.

Mavazi yake ya hio siku yalitiliwa shaka kwani si kawaida yake kama anavyojulikana kuvaa hivyo.

Baadhi ya wanamitandao hawakubaki nyuma na kuanza kuzungumzia mabadiliko katika  mavazi 

Hizi  baadhi ya ujumbe waliomwandikia mwimbaji huyo ni kama zifuatazo:

@barbierbentar- tusweater ndio fom sikuizi mamaaa

@itz-ndeda- tunajua mbona umevaa sweeter

@ben_ndeda "we need front view"

@ritta_abby - "pongezi baby shower loading