Omosh amegeuka kuwa watchie? Video inayomuonyesha akiwa amevalia sare ya mlinzi yazua gumzo mitandaoni

Muhtasari

•Katika video hiyo, Omosh anaonekana akiwa ameegemea ukuta wa duka moja na kusikika akijibizana na jamaa aliyemrekodi.

Omosh amegeuka kuwa Watchie?
Omosh amegeuka kuwa Watchie?
Image: HISANI

Mwigizaji Joeph Kinuthia almaarufu kama Omosh kwa mara nyingine amezua gumzo moto mitandaoni baada ya video inayoonyesha akiwa amesimamia lango huku akiwa amevalia mavazi ya mlinzi kuibuka.

Katika video hiyo, Omosh anaonekana akiwa ameegemea ukuta wa duka moja na kusikika akijibizana na jamaa aliyemrekodi.

Mwigizaji huyo wa zamani wa Tahidi High anasikika akimtumia maneno makali jamaa huyo punde anapogundua kwamba anarekodiwa.

"Wee kijana, unafanya nini hapo? Huo muda wote na hakuna kitu unanunua? Ni kurecord unarecord?.. wee unaona nikiwa nimevalia nini? Hii ni kanzu? Maliza kitu unafanya uinue!" Omosh anasika akisema kwa hasira.

Baada ya video hiyo kuchapishwa mitandaoni Wakenya hawajachelewa kutoa hisia zao kuhusiana na hatima ya mwigizaji huo.

@eddiebutita Hizi script mbaya hivi wasanii mnaandikiwa na nani?

@bienaimesol: Piga kazi eeh, Mkulima sichagui jembe, Mzigo wangu wacha nibebe....

@shaqtheyungin Acheni kuhukumu, hatuko Hollywood!

@_naughty.kid _ Mboka ni mboka

@ephytrap Huyu jamaa aki anataka nini??

Mwigizaji huyo amekuwa akiangiziwa sana mitandaoni mwaka huu tangu alipojitokeza kuomba msaada kutoka kwa Wakenya akidai kwamba alifilisika baada ya kuacha uigizaji.

Wakenya walijitolea kumsaidia kwa kumchangia pesa, mahitaji mengine na hata kumjengea nyumba.

Hata hivyo mwigizaji huyo alikera wengi baada ya kujitokeza na kuomba msaada kwa mara nyingine licha ya kusaidiwa sana katika kipindi cha kwanza.