Amber Ray asherehekea siku ya kuzaliwa ya Jimal Rohosafi huku Amira akiipuuza

Muhtasari

•Amira ameonekana kupendelea kuchapisha matangazo ya kibiashara badala ya kumpakia mfanyibiashara huyo ambaye alitishia kutaliki takriban mwezi mmoja uliopita.

Amber Ray, Jimal Rohosafi, Amira
Amber Ray, Jimal Rohosafi, Amira
Image: INSTAGRAM

Mwenyekiti wa muungano wa wahudumu wa matatu  jijini Nairobi Jamal Marlow Rohosafi anasherehekea siku yake ya kuzaliwa hivi leo. (Desemba 31)

Mamia ya wanamitandao wamejitokeza kusherehekea pamoja na mfanyibiashara huyo hukuwakimwandikia  jumbe nzuri za kheri ya kuzaliwa.

Mwanasoshalaiti mashuhuri Faith Makau almaarufu kama Amber Ray hajaachwa nyuma katika kumsherehekea baba huyo wa watoto wawili na ambaye anaaminika kuwa mpenzi wake.

"Kheri za siku ya kuzaliwa mwenyekiti.. cheers kwa nyingi zaidi" Amber Ray amemwandikia Jimal.

Mke wa Jimal, Amira hata hivyo ameonekana kupuuzilia siku hiyo maalum maishani mwa baba ya watoto wake wawili.

Kwenye ukurasa wake wa Instagram, Amira ameonekana kupendelea kuchapisha matangazo ya kibiashara badala ya kumpakia mfanyibiashara huyo ambaye alitishia kutaliki takriban mwezi mmoja uliopita.

Mnamo mwezi Novemba Amira alielekea mahakamani akiomba kutenganishwa na Jimal baada yake kumsherehekea Amber Ray alipokuwa anaadhimisha siku yake ya kuzaliwa.

Inaaminika kwamba Jimal na Amber Ray wamerudiana baada ya kutengana mapema mwaka huu. Siku za hivi majuzi wawili hao wamekuwa wakionekana pamoja mara nyingi.