Eric Omondi adai ana vitu vilivyoibiwa kutoka kwa Bien katika tamasha ya Konshens

Muhtasari

Vitu ambazo Erick alionyesha kwenye kanda   hio zilikuwa  simu dogo ya 'mulika mwizi' , kifaa cha kinyolea na chupi ya mwanamke.

Image: INSTAGRAM// ERIC OMONDI

Mchekeshaji Eric Omondi  kupitia kanda ya video amedai  ako na vitu mwanamuziki wa kikundi cha Sauti Sol, Bien alipoteza katika tamasha ya Konshens iliyofanyika Carnivore  mnamo Desemba 31 .

Kupitia kwa video aliyopakia  Instagram, Omondi alitaja na kuonyesha  vitu kadhaa  ambazo anadai ni za msanii  huyo. Cha kushangaza ni kuwa vitu zenye mcheshi huyo  alionyesha vitu zaidi ya zile Bien alitaja kapoteza.

Mcheshi Eric  alidai kwa simu ambayo anadai alichukua kutoka kwa Bien hakukuwa na 'voice notes' alizotaja mwanamuziki huyo katika tangazo lake.

"Kama umeishiwa na  mawazo umekosa maangoma, umepanic! usinitumie kusema album yako imeibiwa . Album gani imeibwa? ..hizo vitu niko nazo zote,. ngoma zinawekwa kwa kompyuta kwa studio si kwenye simu. kama umeishiwa na  mawazo .. acha woga, tafuta mtu akuandikie mangoma. kujia vitu zako Bwana," alisema.

Vitu ambazo Erick alionyesha kwenye kanda   hio zilikuwa  simu dogo ya 'mulika mwizi' , kifaa cha kinyolea na chupi ya mwanamke.

Bien alipotangaza kwamba alipoteza vitu vyake vya thamani katika tamasha ya kufunga mwaka Carnivore ambayo ilihudhuriwa na mwimbaji wa Jamaika Konshens na kutoa zawadi ya Ksh 50,000 kwa yeyote atakeyezipata vitu hizo.